Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la uzalishaji la Suma JKT Kanali Petro Ngata akizungumza na waandishi wa habari katika maeneo ya shamba darasa.
NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA
JESHI la kujenga Taifa (JKT),limesema kuwa lipo mstari wa mbele kuhakikisha wanafanya kilimo bora chenye mfano kwa jamii ndio maana.wameweka shamba darasa ili wananchi waje wajifunze kwa kuwa kilimo kina tija.
Pia amewataka wananchi kujitokeza katika maonyesho ya kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea jijini Mbeya ili kuwaspata elimu katika shamba Darasa la Jeshi hilo la mazao mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya kutembelea shamba hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la uzalishaji la Suma JKT Kanali Petro Ngata amesema jamii inapaswa kuja kupata elimu ya namna ya mboga yanavyolimwa na kutunzwa ili msimu ujao waweze kula kilimo chenye tija.
Kanali Ngata ameeleza zaidi ya kuwa Jeshi hilo liko mstari wa mbele kuhakikisha wanafanya kilimo bora chenye mfano kwa jamii mdio maana.wameweka shamba darasa ili wananchi wakajifunze.
"Wanamchi jitokezeni katika shamba darasa la JKT lenye mazao mchanganyiko ambalo wanaweza kujifunza ili wakalime katika maeneo yao,"amesema Kanali Ngata.
Kanali Ngata ameeleza kuwa ongezeko la bajeti kwenye sekta ya kilimo itasaidia kupanua wigo kwenye sekta hiyo ili wakulima wazidi kupiga hatua na kufanya kilimo chenye tija.
Amesema bajeti huyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa uzalishaji mkubwa katika mazao mbalimbali yakiwemo ya mazao ya chakula kama mahindi,Mpunga na mengine.
Naye Mkurugenzi wa Kilimo na Uvuvi wa JKT Kanali Peter Lushika amesema wamekuja na teknolojia mpya ya namna ya ufugaji wa samaki katika mabwawa,Vizimba na mabwawa na matenki na la kufanya hivyo ni pamoja na.kiwaaogezea hudua ya upatikanaji wa samaki aina ya sato kwa urahisi katika maeneo mbalimbali tofauti na kusubiri sato kutoka mkoa wa Mwanza pekee.
Ameongeza kuwa JKT ipo mstari wa mbele kuhakikisha kilimo wanachofanya kinakuwa na maslahi kwa jeshi hilo na taifa kwa ujumla.
"Haturudi nyuma kwenye kilimo kila iitwapo leo,tunazidi kusonga mbele kutokana na teknolojia tunayotumia kwenye kilimo,"alisema Kanali Rushika.
Amesema wameahiriki katika maonyesho hayo ili kuweza kutoa elimu lwa wakula na wafugaji kutokana na wao kuwa webobea katika sekta hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho ya Nane Nane Kanali Shija Lupi ametoa wito kwa wakulima kufika katika shamba darasa la JKT ili kujifunza namna ya utunzaji wa mazao tokea kupanda hadi kuvuna.
Amesema teknolojia wanayofundisha wakula wanaotembelea katika banda hilo,itawasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga hatua katika kilimo wanachofanya.
0 Comments