Na Asha Mwakyonde Mbeya
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA),Dk Stephan Ngailo amesema serikali imeandaa mfumo wa kielektroniki ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuziba mianya ya ubadhilifu katika utoaji wa ruzuku za mbolea kwa wakulima nchini hivyo wasambazaji.wasitarajie kupata chochote,"alisema Dk Ngailo.
Pia amesema kuwa wanatarajia Agosti 15 na 16 mwaka kutangaza tenda ya ruzuku ya mbolea kwa wakulima nchini na kwamba serikali imeweka na kuimarisha mfumo imara wa utoaji mbolea ya ruzuku kwa wakulima katika kwenye msimu ujao wa kilimo ili kuziba moanya ya ubadhilifu.
Akizungumza katika maonyesho ya Nane Nane kitaifa jijini Mbeya jijini Mbeya Dk Ngailo alisema,lengo ni kuhakikisha wakulima wanufanika na mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuondoka kero za awali zilizojitokeza katika mifumo ya ruzuku iliopita.
" Serikali imejiwekea mfumo imara na bora ya utoaji wa ruzuku za mbolea ambao utasaidia kuwafikia wakulima na hii itaondoa au kuziba mianya ya Watu wasio waadilifu katika suala utoaji ruzuku hii," amesema.
Ameongeza kuwa serikali imejipanga vema kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati katika msimu huku akiwataka wakulima kujitoleza kujisajili kwenye mfumo huo ili waweze kupata mbolea hiyo ya ruzuku.
Dk.Ngailo amefafanua kuwa kupitia mfumo huo usambazaji wa mbolea za ruzuku utatolewa na mtu sahihi na
kumfikia mkulima kwa wakati .
Amesema Usajili utafanywa na Afisa ugani waliopo katika ngazi za kata na vijiji na ku na Mwenyekiti wa kijiji na baadaye taarifa za mkulima
kuingizwa katika mfumo wa kielectroniki ili kuwezesha usambazaji wa
mbolea hizo.
Ameongeza kuwa,mzalishaji au mwingizaji wa mbolea nchini
atatumia mifuko maalum kwa ajili ya ruzuku yenye QR code na maandishi
yanayosomeka ruzuku ili kuutambulisha kuwa mbolea hiyo inanunuliwa na
mkulima kwa bei ya ruzuku.
Dk. Ngailo utoaji wa ruzuku za mbolea ni matokeo ya maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kuona umuhimu wa kuwawezesha wakulima kulima kwa tija na kupelekea uhakika wa mavuno ya chakula na biashara kwa ustawi wa jamii
na taifa kwa ujumla.
Kutokana na hilo kiasi cha shilingi bilioni 150 za kitanzania
zimetengwa ili kutumika kutoa mbolea za ruzuku kwa wakulima kwa Mwaka
wa Fedha 2022/2023.
0 Comments