NA ASHA MWAKYONDE,DAR ES SALAAM
AFISA Ushirika wa vyama vya kuweka akiba na mikopo (SACCOS), kutoka Wilaya ya Ubungo jijini hapa Joseph Mkotya amesema kuwa wanajivunia kuwa na Chama cha Ushirika cha Awape SACCOS LTD kwa kuwa kinafuata miongozo wa serikali.
Pia ameishauri SACCOS hiyo kufanya jidihada za kuhamasisha zaidi wanachama wapya wajiunge na endapo wakiomba msaada wa kuweza kusaidiwa kwa kuitisha mikutano ya hadhara kutoa elimu na faida ya vyama vya ushirika kwani wengi hawajajiunga kutokana na kutokuwa elimu hiyo.
Hayo ameyasema jijini hapa Septemba 30, 2022 katika mkutano mkuu wa chama hucho, Mkotya amesema Awape SACCOS kinaenda vizuri kwa kuwa kinafuata misingi na muongozo wa serikali na kwamba ni hatua nzuri waliofikia ya kuunda SACCOS hiyo licha ya kuwa ni chama cha akina mama walea pekee.
"Tunajivunia Awape SACCOS kama wanahisa kwa kuwa ni chama kinachoenda vizuri kinafuata miongozo ya serikali ndio maana kinatupa matumaini ya kuendelea kuwepo," amesema Mkotya.
Ameongeza kuwa SACCOS ni sehemu pekee ya kuhakikisha wanachama wanajikwamua katika maisha magumu, na kwa kuwa wanachama hao ni akina mama walea pekee wanaamini asilimia mia moja wataboresha maisha yao kwa kutumia nguvu ya pamoja.
Aidha ametoa wito kwa wanachama hao kujenga tabia ya kurejesha marejesho yao kwa wakati ili yaendelee kuwasaidia na kukuza mtaji wao wa hisa.
Awali Mwenyekiti wa muda wa mkutano huyo Mwashabani Athuman amewashukuru wanachama kwa kuuliza maswali yenye lengo la kukijenga chama hicho.
0 Comments