WIZARA YA AFYA YASAINI MIKATABA 7 KWA AJILI YA MASHIRIKIANO YA KIMATAIFA KUHUSU MAFUNZO YA WATALAAM , TIBA, TAFITI NA UWEKEZAJI


 Na WAF- Dodoma 

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameweka wazi kuwa,  Serikali kupitia Wizara ya Afya imesaini hati za makubaliano saba (7) kwaajili ya mashirikiano ya kimataifa katika kuboresha huduma za afya kwa Watanzania. 

Prof. Makubi amesema hayo leo katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, tukio lililoambatana na usainiaji wa Mkataba wa saba na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Alameda Bw. Neeraj Mishra iliyopo nchini Misri na kuhudhuriwa na Waandishi wa habari.

Ametaja, Hospitali zilizo katika makubaliano hayo ni pamoja na Hospitali ya MIOT ya nchini India, Hospitali ya Sheba ya nchini Israel, pamoja na nchi za Uturuki, Kenya, Burundi, Rwanda na Hospitali ya ALAMEDA iliyo nchini Misri. 

Aidha,  Prof. Makubi ameweka wazi kuwa, hati hizo za makubaliano zimelenga kuimarisha mahusiano katika mafunzo kwa watumishi wa afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi ambapo zaidi ya Wataalamu 20 hufaidika kila mwaka kwa gharama nafuu.

Ameendelea kusema kuwa, makubaliano hayo yamelenga kubadilishana Wataalamu ambapo watapata fursa ya kwenda kujifunza nje ya nchi, pia Wataalamu wa nje kuja kufanya kazi na Wataalamu wetu  wa ndani ya nchi.

Pia makubaliano hayo yamelenga mashirikiano ya kikanda katika masuala ya udhibiti wa magonjwa ya dharura mipakani, masuala ya tafiti za tiba na kinga, huduma za tiba mtandao na Tehama, pamoja na viwanda vya dawa na vifaa tiba. 

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA