eGA KUWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA MTANDAO


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA),
imepanga kuweka mwelekeo wa Serikali katika kuandaa na kutekeleza mikakati madhubuti lengo ikiwa ni kufikia uwezo wa kutumia teknolojia mpya zinazoibuka hasa zile za akili bandia na sarafu za kidijitali na teknolojia za kifedha.

Akizungumza jijini leo Februaro 6, 2023 Jijini Dodoma wakati  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Benedict Ndomba katika kuelekea kikao kazi cha 3 cha Serikali mtandao ambacho kinatarajia kufanyika Jijini Arusha  Februari  8 Hadi 10 mwaka huu.

Mkurugenzi huyo amesema kikato hicho kitawakitanisha wadau zaidi ya 1000
ameeleza kuwa wamejipanga kuandaa na kutekeleza sehemu moja ambayo huduma ya Mitandao zote zinakua zinapatika kwa urahisi.

Mhandisi Ndomba amefafanua kuwa  lengo kubwa ni kuwakutanisha wadau hao  mbalimbali wa Serikali Mitandao ili kujadiliana juu ya mafanikio ,changamoto pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza Serikali mtandao, matumizi sahihi na salama ya TEHAMA katika Taasisi za Umma.

"Tunatarajia kupokea wa 1000 kutoka mashirika na Taasisi za Umma wakiwemo maafisa Masuhuli ,wajumbe wa Bodi ,wakuu wa vitengo vya TEHAMA maafisa TEHAMA,maafisa Rasilimali watu,Maafisa mipango ,maafisa Mawasiliano,wahasibu pamoja na watumishi wote wa mifumo ya TEHAMA Serikali hao wote wanatarajia kushiriki kikao kazi hiki," amesema.

Amesema mamlaka hiyo imepanga kuhakikisha taasisi zote za Umma wakiwemo maafisa Masuhuli ,wajumbe wa Bodi ,wakuu wa vitengo vya TEHAMA maafisa TEHAMA,maafisa Rasilimali watu,Maafisa mipango ,maafisa Mawasiliano,wahasibu pamoja na watumishi wote wa mifumo ya TEHAMA Serikali hao wote washiriki kikao kazi hicho lengo  ni kufanya mifumo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU