RAIS DK. SAMIA AFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA UJENZI, BARABARA KUPIMWA KWA KUTUMIA MITAMBO

Na Asha Mwakyonde Dodoma

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Akson amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya uwekezaji wa eneo la miundombinu ya Barabara ikiwamo kuiwezesha fedha Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS),kununua mitambo na vifaa vya kisasa hivi karibuni ambapo wakala huo utaisaidia serikali kuondokana na changamoto ya kukabidhiwa miradi ya barabara iliyo chini ya kiwango.

Pia  ameisisitiza wizara hiyo  kupitia TANROADS kuhakikisha miradi yote ya  barabara inayokamilia inapimwa ubora kwa kutumia vifaa hivyo vya kisasa kabla mkandarasi kuikabidhi kwa serikali.

Akizungumza  leo Mei 27, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akifungua Maonesho ya siku mbili ya wizara hiyo  na taasisi  zilizo chini yake katika viwanja vya Bunge amesema awali  kulikuwa na matumizi yasiyoridhishwa ya fedha za walipa kodi kutokana na baadhi wakandarasi kukabidhi barabara chini ya kiwango.

Dk.Tulia ameeleza kuwa mvua zikinyesha kipindi kimoja zinaweka mashimo na kufanya wabunge kuanza kutafakari namna ya kuishauri, kusimamia kwamba imejengaje barabara kama hiyo.

"Tunafahamu miaka miwili iliyopita Rais Dk Samia alipewa tuzo katika eneo la miundombinu ya barabara bila shaka tuzo ile inaonesha namna ambavyo tumepiga hatua," amesema.

Dk.Tulia ameongeza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk.Samia Wizara ya Ujenzi imetimiza kile ambacho Watanzania wanakihitaji

Ameeleza kuwa tatizo halikuwa  ujenzi bali ukosefu wa teknolojia ya kupima udongo tangu mwanzo wa kazi ambapo kwa sasa hali hiyo haitajitokeza huku akiwaomba wataalamu kutumia teknolojia hiyo kupokea miundombinu iliyokamilika.

Akizungumzia  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),amesema kwa namna Tanzania ilivyo kubwa, kuna haja ya kuwa na magari mengi ya Karakana zinazotembea na kuendelea kupokea ushauri unatolewa na Bunge ili waipatie Serikali mapato kutokana na utendaji kazi wao mzuri licha ya kuwa anatambua kuna changamoto nyingi katika Taasisi hiyo

 "Namewapongeza kwa kufanya mageuzi ya kuwatafuta wateja waliko na kufanya kazi ya matengenezo kwa saa 24 kwa kutumia Karakana zinazotembea (Mobile Workshop), kuliko ilivyokuwa awali ambapo mlisubiri kupelekewa kazi za kufanya kwenye maeneo yenu," ameeleza.

Awali,  Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akimkaribisha Spika, amesema kumekuwa na mageuzi makubwa ndani ya Wizara hiyo kutokana na uwezeshwaji mkubwa wanaoupata kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Bashungwa amesema wamejipanga ndani ya Wizara hiyo katika kuwahudumia Watanzania ili lengo la kiongozi mkuu wa nchi katika Sekta ya Ujenzi liweze kutimia.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI