WAZIRI NDEJEMBI: TK MOVEMENT IPEWE USHIRIKIANO KUKUTANA NA VIJANA WENZAO


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WAKUU wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Kata, Mitaa, Vijiji, Taasisi na Asasi mbalimbali wameombwa kuwapa vijana  wa TK  Movement ushirikiano wa kutosha wanapopita katika maeneo yao kukutana na vijana wenzao kubadilishana mawazo na kuwapa mafunzo ya namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa.

Hayo ameyasema leo Mei 25,2024  jijini Dodoma  na Waziri wa Nchini, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu na  Deogratias Ndejembi wakati akizindua Mtandao wa Kitaifa wa Vijana wa  Taifa Letu, Kesho yetu iliyobora (TK Movement), amesema ushirikiano huo unalenga kuwapatia vijana waliopo pembezoni mwa mikoa fursa zilizopo katika maeneo yao pamoja na kuendelea kuyazungumzia mema na mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya sita.

Ameeleza kuwa kwa sababu hiyo, haoni  sababu ya kukataa ombi hilo la kupatiwa ushirikiano na viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnapofanya ziara kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwahamashisha na kuwaelimisha vijana wenzenu.

Waziri huyo amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya sekta binafsi kukua kwa kuweka vivutio vya kikodi na kurahisisha uwekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi kwa lengo la kutanua fursa za ajira kwa vijana na wanawake.

"Ni ukweli usiopingika kuwa Serikali haiwezi kuajiri vijana wote wanaohitimu elimu ya juu, na hili mmekiri wenyewe kwenye risala yenu kuwa kati ya vijana 800,000 wanaoingia kwenye soko ala ajira kila mwaka, ni vijana 40,000 pekee wanaopata ajira rasmi ikiwa ni sawa na asilimia 5 tu," amesema.

Ameeleza kuwa kutokana na ukweli huo mchungu, ni lazima vijana muanze kubadili fikra kuwa,maisha si kuajiriwa pekee kama walivyopendekeza wenyewe, na mimi nawaunga mkono, ni lazima muanze kuzitambua na kuzitumia fursa zinazowazunguka katika kuboresha maisha yenu.

Waziri huyo amesema Serikali, jukumu lao litakuwa ni kujenga mazingira rafiki na wezeshi ili vijana na wanawake waweze kuzifikia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika halmashauri zetu. 

"Mathalani, miradi ya maendeleo inapotekelezwa katika ngazi za Halmashauri, ni muhimu Wakuregenzi wetu wa Halamashauri wakatoa hamasa na kipaumbele  kwa vijana na wanawake  kuchangamkia fursa za ajira zitakazokuwa zinaambatana na miradi hii, amesema.

Naye  Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema kuwa serikali inaunga nguvu zote zinazofanywa na vijana  huku akisema ni lazima vijana hao wajue mambo ambayo yanyafanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

" Tumpende mama ,tuipende Tanzania kama tunavyopenda michezo hivyo umoja huu uendeleze ushirikiano wenu bila kujali itikati za vyama," amesema Zungu.

Akizungumzia uchanguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwaka huu Naibu Spika huyo ameeleza kuwa hawawezi kupata viongozi bora endapo vijana hao hawatajitokeza kupiga kura.

Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa mtandao huo Alice Erasto amesema kuwa lengo Tk Movement ni kutengeneza mtandao imara wenye nguvu na ushawishi ili kiwaleta pamoja vijana na wanawake katika kujenga mtazamo chanya juu ya mustakabali  wao na kuhakikisha mgao sawa wa rasilimali katika nchi na haki ya kila raia.

"Kwa kuwa maendeleo ya nchi yanategmea sana vipaumbele vya serikali vilivyoainishwa kwenye mpanga kazi wa Taifa wa Maendeleo ya miaka mitano na kwa kuwa mipango hii hutekelezwa kwa kutumia bajeti ya serikali huindhinishwa na Bunge katika Kila mwaka wa fedha," amesema.

Ameongeza kuwa zipo fursa nyingi za kiuchumi kwa vijana na wanawake kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia ambayo imejipambanua katika kukuza uchumi na kuongeza bajeti ya miradi ya kimaendeleo kila sekta kwa miaka minne mfuliizo.

Alice ameeleza kuwa ndoto yao vijana na wanawake wa Tanzania ni kuwa na kesho iliyobora  kuliko leo  na kwamba huo ndio msingi wa mtandao huo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU