TASAF YAJIPANGA KUTOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, WANANCHI WASHAURIWA KUTEMBELEA


Waziri wa Inchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Tasaf katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanj a vya Chinangali Park Jijini Dodoma.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF), umesema umejipanga kutoa elimu kuhusu mfuko huo kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea katika banda la TASAF kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma ili waweze kupata uelewa zaidi wa mfuko huo.

TASAF nibMpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo lengo kuu la mpango huo ni kuzipatia ruzuku kaya za walengwa ili ziweze kuboresha hali zao za maisha na kuweza kuwekeza katika shughuli za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato cha kuwawezesha kumudu mahitaji yao muhimu ikiwemo Afya, Lishe, Elimu na kuwasaidia kuondokana na umasikini katika kaya hizo.

Akizungumza leo Juni 19,2024 katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Nchini yanayofanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Chinangali Park Mkurugenzi wa mawasiliano na Mfumo wa Mfuko wa TASAF, Japhet Boazi amesema Wiki hiyo ni fursa nzuri kwaob ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kuisikiliza malalamiko wote wenye changamoto mbalimbali kuhusu mfumo huo ambapo watapatiwa ufumbuzi wa kina.

"TASAF imekuwa ikisaidia kaya maskini kwa kuwapa mitaji na mafunzo mbalimbali kama ya ujasiriamali na wanapofanikiwa kusimama wenyewe tunawaacha wajitegemee ," ameeleza.

Ameongeza kuwa mpango wa TASAF umeleta mabadiliko mengi katika jamii na kwamba wanufaika wake ni wengi ambapo wamejikita katika masuala ya ujasiriamali ikiwamo wa kilimo ufungaji na hata ule wa kutengeneza bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake mnufaika wa TASAF Kuruthumu Abdallah amesema mfuko huo umebadilisha maisha yake tofauti na awali alivyokuwa akipata mlo mmoja kwa siku.

Ameeleza kuwa TASAF imempatia elimu pamoja na mtaji wa kuanzisha biashara yake iliyomfikisha katiia hatua ya kujitegemea.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI