Na Asha Mwakyonde, DODOMA
"TUNAJIVUNIA kuwa na kiongozi mwanamke Rais Dk.Samia Suluhu Hassan mwenye maono, amefanya vitu vingi hakuna Sekta inayokwama katika kutekeleza majukumu yake kwa jamii.
Hayo si maneno yangu bali ni ya Mwenyekiti Jukuwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma Salama Salumu wakati akizungumza na mwandishi wa makala haya.
Mwenyekiti huyo anaushukuru uongozi wa Rais Dk.Samia huku akisema ni kiongozi mwanamke shupavu,mahiri na makini katika kutekeleza majukumu yake ya Kitaifa.
Akizungumzia Jukwaa hilo Salama anaeleza kuwa liameanzisha na Rais Dk.Samia kwamba aliona ni vema kuwaunganisha wanawake kupitia Wazari ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Anasema kuwa Rais Dk.Samia alipoingia madarakani katika nafasi ya juu ya Rais amekua ni mama makini, mahiri na ni mama mwenye misimamo huku akieleza ni mfano wa kuingia na dunia sio Tanzania kutokana na uongozi wake mzuri.
SEKTA YA AFYA
Akizungumzia Sekta ya afya Salama anasema huduma zinazotolewa ni nzuri kuanzia ngazi ya zahanati,vituo vya afya, hospitali za Rufaa za mikoa na zile zinazopokea Rufaa.
"Huduma za dawa na vifaa tiba zinapatikana kwa wakati na endapo vitakosekana ni kwa kuchelewa kufika sehemu husika tu na si vinginevyo," anasema.
Hata hivyo, Mei 13, 2014/2025 Bunge lilipitisha bajeti ya wizara ya afya ambapo jumla ya shilingi trilioni 1.3 ilipitishwa na Bunge hilo ikiwa ni ongezeko la shilingi Bilioni 76.5 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24, sawa na ongezeko la asilimia 6.
MIUNDOMBINU
Salama anasema Rais Dk Samia amesimamia miundombinu ya barabara ambapo wanasafiri bila changamoto yoyote na wanafika kwa wakati kutokana na miundombinu hiyo kuboreshwa tofauti na awali.
"Kwa sasa sisi wakulima barabara zinapitika vizuri na tunasafirisha mazao yetu kutoka shambani hadi nyumbani pia hata wanunuzi wa mazao yetu wanatufikia kwa urahisi," anasema Mwenyekiti huyo.
Anafafanua kuwa Rais Dk. Samia ni mchapa kazi ambapo watanzania wanasafiri kwenda popote hapa nchini bila kukwama katika kipindi hiki cha uongozi wake.
Mwenyekiti huyo anaongeza kuwa katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dk.Samia wao kama wanawake wanafanya biashara na faida wanazipata kutokana na ubora wa miundombinu ya barabara.
Akizungumzia miundombinu ya umeme anaeleza kuwa umeme huo umezifikia hadi nyumba za tembe maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kwamba gharama yake ni nafuu.
"Upatikanaji wa umeme vijijini vijana wengi wamejiajiri kupitia umeme huu, tunaona wanvyotengeneza, kuchomelea mageti na madirisha kwa kutumia umeme tofauti na awali mtu anayejenga ilikuwa ikimlazimu kwenda mjini kununua mageti haya," anasema.
Anaongeza kuwa hata saluni za kike na kiume zimeongezeka maeneo ya vijijini huku akisema mafundi wa kushona nguo nao wameongezeka ambapo wanatumia mashine za umeme.
Salama anasema kutokana na jitihada za Rais Dk.Samia katika utendaji kazi wake watanzania wengi wanamuamini.
Anasema kwenye suala la elimu Rais Dk Samia ameweza kuboresha miundombinu kwa kujenga shule, kuongeza vifaa vya kufundushia pamoja na kuongeza walimu.
Mwenyekiti huyo anasema kwamba kwa sasa hakuna mwanafunzi anae maliza darasa la saba hauwezi kusoma na kuandika kama awali.
"Siku hizi hakuna sifuri nyingi kwa shule za sekondari nitolee mfano wa shule ya sekondari ya Ula iliyopo hapa Kondoa ambapo kabla ya Rais Dk.Samia kuingia madarakani kulikuwa na sifuri 95 na kwa sasa kuna sifuri tano tu," anasema na kuongeza kuwa:
Rais Dk.Samia anaweza kuongoza nchi kusingekuwa na katiba ya nchi Rais huyu angeweza kuwa Rais wa milele," anasema.
Aidha, akizungumzia suala la usafiri salama anaeleza kuwa awali kulikuwa na changamoto ya usafiri ambapo watanzania walikuwa wakisafiri saa 12 kufika wanapokwenda lakini kwa sasa treni ya mwendosi imerahisishia kwa wanaokwenda Dar es Salaam kununua bidhaa.
Salama anafafanua kutokana na kurahisishwa kwa usafiri uchumi wa nchi utaongezeka kwa kuwa wafanyabiashara wanatumia muda mchache kununua bidhaa Dar es Salaam na kurudi ambapo wanaendelea na biashara zao bila kupoteza muda wao.
"Rais Dk.Samia ni mchapa kazi ,halali anafuatilia jumbe zinazotumwa na wananchi wake mitandao na anazijibu kwa vitendo, tunamshukuru mama kwa upendo wake," anaeleza Mwenyekiti huyo.
Anasema Rais Dk.Samia amewainua wanawake katika kila Sekta wanawake hao wananafasi katika uongozi huku akisema kwa sasa wanawake hawana vilio vya kiuchumi.
" Sisi wanawake tunamuahidi 2025 kura zote kwa mama Samia na za kishindo kwa kuwa anatufanyia mengi na kwamba awali kwenye siasa hapakuwa na wanawake wengi kwa sasa wapo wengi, timekuwa na nguvu ya kujitetea, kujisemea tofauti na mwanzo.
Naye Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Singida Asha Mwandala anasema kuwa uongozi wa Rais Dk.Samia umeboresha miundombinu mbalimbali ikiwamo ya barabara,Sekta ya Elimu na nyinginezo.
" Natoa pongezi nyingi kwa Rais Dk. Samia kwa kutekeleza kila mradi kwa kiwango na kwa wakati .Ukiangalia miundombinu ya barabara zimechongwa nchi nzima na nyingine zimejengwa kwa kiwango cha lami hata katika upande wa elimu shule zumeongezeka kila kata," anaeleza Mwandala.
Anaongeza kuwa Rais Dk.Samia amepambana na ufisadi,amekuza sekta ya utalii,ameboresha sekta ya afya huku akisema watanzania wanajivua kupata Treni ya umeme ambapo hawakutegemea kuanza kufanya safari zake kwa wakati.
0 Comments