GCLA YATOA ELIMU YA KEMIKALI KWA WAJASIRIAMALI SABA SABA


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

MKURUGENZI wa Huduma za Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamalaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GGLA),

Dk.Peter Shimo amesema mamlaka hiyo ipo katika maonesho hayo kwa ajili yakuendelea kutoa elimu ya masuala mbalimbali hasa ya katika masuala ya kemikali.

Pia amewataka wajasiriamali wanaojishughulisha na kemikali kufika katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa Biashara Dar es Salaam (DITF), kwa lengo la kupata elimu kuhusu kemikali pamoja na kufanya usajili wa bidhaa.

Hayo ameyasema leo Julai 5, 20225 katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba' amesema huduma wanazozitoa kwenye banda lao ni pamoja usajili wa kemikali.

"Wahusika wanaofika hapa katika banda letu wanapata elimu kuhusu shughuli zetu tunazozifanya," alisema Dk. Shimo.

Ameongeza kuwa lengo la mamalaka hiyo ni kuhakikisha jamii inapata elimu ya kemikali na mambo mengine yanayohusiana na mamlaka katika maeneo yote.

amesema mamlaka pia ina mfumo wa kusajili wajasiriamali mtandaoni kwa ajili ya watu ambao wapo mbali na watoa huduma hiyo.

Post a Comment

0 Comments

KIKKIDES AWATAKA VIJANA KULINDA AMANI, AONYA KUHADAIWA NA MITANDAO