RAIS DK. SAMIA KUWA MGENI RASMI MKUTANO MKUU BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MKUTANO  Mkuu wa 79 wa  Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) unatarajia kufanyika Mei 19 mwaka huu huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa Mkutano huo na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi .
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo Februari  20,2024 jijini Dodoma Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Baraza hilo  Meja Jenerali Francis Mbindi alisema kuwa lengo la mkutano huo ni  kutumia shughuli za michezo na utimamu wa mwili kama njia ya kueneza amani duniani, huku tunu za baraza ikiwa ni kuhamasisha mshikamano, urafiki, heshima, usawa, uadilifu na ushupavu. 
 
Amesema,Tanzania imepata heshima ya kuandaa mkutano huo kutokana na kukidhi  vigezo ikiwemo kupatikana kwa huduma staki pamoja na amani na utulivu uliopo nchini.
 
Ameeleza,mkutamo huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam una wanachama kutoka nchi 140 huku akisema nchi zote wanachama wanatarajiwa kushiriki ambapo mbali na kushiriki mkutano huo wajumbe watapata fursa ya kutembelea mnara wa kumbukumbu ya mashujaa walioipigania Tanzania, kutoa heshima na kuweka mashada ya maua kama ishara ya kuwaenzi mashujaa hao.
 
Meja Jenerali Mbindi amesema,uji huo utakuwa na manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kulitangaza Jeshi la Wananchi wa Tanzania,kutoa fursa kwa lugha adhimu ya Kiswahili kwani itakuwa ni miongoni mwa lugha tano zitakazotumika katika mkutano huo.

Amefafanua kuwa mkutano huo utatoa fursa ya kiuchumi ambapo wafanyabiashara mbalimbali watapata fursa ya kufanya biashara zao na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
Amesema,kwa mara ya pili Tanzania inapata fursa ya kuandaa mkutano huo ambapo mara ya kwanza ni mwaka 1991 ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walitembelea mbuga za wanyama na hivyo kutangaza utalii nchini na kuingiza kipato kupitia sekta hiyo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU