MWAKAGENDA AHAMASISHA WANAWAKE KUCHUKUA FOMU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Na Asha Mwakyonde,Geita

MBUNGE wa Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda amewataka wanawake nchini kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji unatarajiwa kufanyika mwaka huu ili kuendana sambamba na Rais DK.Samia Suluhu Hassan kutekeleza majukumu yake.

Hayo ameyasema Machi 9,2024 mkoani Geita katika kongamano la wanawake wachimbaji wadogo wa madini amesema mwanamke ni kiongozi kiasili anaongeza kuanzia ngazi ya familia.

Mbunge Mwakagenda ameeleza kuwa Mkoa wa Geita una wanawake wachimbaji  ni wengi kuliko sehemu mwingine yenye wachimbaji wadogo.


"Mkuu wa Mkoa tunaomba ufikishe salamu zetu za wanawake wote wachimbaji, kazi kubwa anayoifanya aendelee kuwasaidia wanawake Taifa letu kwa sasa linasonga mbele na ameweka utulivu wa kisiasa  mimi ni mpinzani nipo chama mbadala sio upinzani lakini kwa sasa tunafanya siasa safi,"amesema

Amefafanua kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kusema na watanzania huku akisema hawawezi kuongea na wanawake nchi nzima ndio maana wameutumia Mkoa huo kuongea na wanawake wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwa wao wataweze kufikisha ujumbe kwa wanawake wengine.


Mbunge huyo amesema kuwa wanampango wa kusimamia madini ambao Waziri wa madini Antony Mavunde ameuelezea 2030 kwamba madini yanafaida kwa mwanamke wa kawaida na kwa Taifa.

Mbunge huyo ameeleza kuwa wanawake hao wamekuwa na faida katika uchimbaji na wamehusika kuongeza Pato la Taifa huku akisema wanaongea nao ili kazi wanazozifanya kusaidia kuongeza uchumi iendane sambamba na kutunzwa mazingira pamoja na kujua idadi yao.

Ameongeza kuwa mwaka 2022 / 2023 wamekuwa fanya mambo ya sensa kujua idadi ya wanawake huku akisema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anapotaka kujua idadi ya wanawake wachimbaji kupata takwimu sahihi ili aweze kuwasaidia.


Awali akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa huo Martin Shigela alisema kuwa harakati za kudai haki za wanawake zilianza muda mrefu na kwamba lazima ziwe endelevu.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema nchi imetoka kwenye harakati za kumkomboa mwanamke na kwamba serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia inampango wa kumuweka mwanamke katika nafasi kubwa ya kiuchumi.

"Sophia Mwakagenda alikuja na  akaniambia natarajia kufanya mafunzo kwa wajasiriamali wanawake hasa nyie wanawake wachimbaji wadogo na leo mpo hapa mtajifunza mambo mengi ni pamoja na kufahamu takwimu," alisema Shigela.

Naye Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa(NBS),Ruth Minja alisema kuwa wamefika mkoani hapo kwa ajili ya kuungana na wanawake wenzao ikiwa ni sehemu ya usambazaji wa mafunzo ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2020 /2022 ambapo sensa hiyo ilikusanya taarifa nyingi ikiwamo ya wanawake.l na aina ya kazi wanazozifanya.

"Nitumie fursa hii ya namna ya kuyatumia matokeo ya sena katika kupanga Maendeleo ya nchi yetu," alisema Mkurugenzi huyo wa takwimu za jamii.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI