MZUNGUKO WA SABA MFUKO WA DUNIA KUTOKOMEZA MAGONJWA WAZINDULIWA DODOMA


 N sha Mwakyonde,Dodoma

WANAOTEKELEZA Mradi wa mzunguko wa saba wa Mfuko wa Dunia (Global Fund 7), wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza tija katika kutokomeza magonjwa ya Ukimwi,Kifua kikuu na Malaria nchini Tanzania ifikapo Mwaka 2030.

Mradi huo umeziduliwa na Wizara ya afya juzi jijini Dodoma ambao 
utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia sasa kwaajili ya kutokomeza magonjwa hayo ambapo unatarajiwa kugharimu dola za kimarekani Milioni 602 Sawa na Fedha za Kitanzania Trioni 1.4.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Dk. John Jingu wakati akuzindua Mradi huo alisema watakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji na kuongeza uwajibikaji kwa lengo la kuboresha hali ya utoaji wa huduma za Afya nchini.

Dk.Jingu amesema fedha hizo zimetokana na jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya ili ziweze kuwafikia wananchi katika maeneo yao bila kikwazo.

Ameeleza ili kufikia malengo haya, wote wana wajibu wa kusimamia na kutekeleza ipasavyo mipango tuliyojiwekea na kuwezesha shughuli zote za mradi ambazo zimepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2024-2026 zinakamilika kwa asilimia mia moja.

"Serikali ya awamu ya sita imewekeza fedha nyingi katika Sekta ya afya kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wake hivyo watumishi hao wafanye kazi zao kwa weledi mkubwa," ameeleza Dk. Jingu.

Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Dk.Tumaini Nagu alieleza kuwa wapo kwaajili yakujipima na kuangalia walipotoka na walipo ili kufika malengo ya Kidunia namba tatu kwa kutekeleza Strategic Plan ya afya namba tano.

Profesa Nagu ameongeza kuwa Serikali imeona umuhimu katika kutokomeza magonjwa haya ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria ili ifikapo Mwaka 2030 kusiwe na tatizo.

Awali Mwakilishi wa Serikali ya Marekani ambao ni wanatekelezaji wa Mradi wa PEPFAR,Getrude Temba alisema wanatambua mchango wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Magonjwa hayo.

Aidha amewasisitiza kufanya kazi kwa umakini katika kuhakikisha rasilimali wanazopatiwa zinatumiwa kwa usahihi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU