VETA KIHONDA YABUNI BUSTANI YA MBOGA MBOGA INAYOTEMBEA

Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),kupitia Chuo cha VETA Kihonda imetengeneza, imebuni bustani ya mboga mboga ya kutembea ambayo inakaa sehemu yoyote katika nyumba.

Akizungumza leo Agosti 2,2025 katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini hapa,Mwalimu Zana za Kilimo na Kilimo kutoka VETA Kihonda Morogoro, Gema Ngoo amesema wanafundisha zana za kilimo na kilimo pamoja na namna ya kutengeneza vifaa pamoja na kufundisha kilimo kisichotumia dawa.

Mwalimu Ngoo amefafanua kuwa wanatengeneza mbolea na kuweka wadudu aina ya minyoo ya kawaida, maji pamoja na uchafu wa vyakula ambapo itakuwa busta inayo mwagiliwa kwenye bustani ya mboga mboga hivyo hazihitaji kunyunyuzia dawa zenye kimikali na mbolea za viwandani.

"Kulingana na kaulimbiu ya maonesho haya isemayo 'Changua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi' kipindi hiki tunajua tanaelekea kwenye uchaguzi Mkuu tunatakiwa tuchague viongozi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu watakaoweza kusimamia VETA vizuri ili vijana wetu waendelee kupata mafunzo vizuri na baadae waweze kujiari wenyewe," amesema.

Aidha aliwakaribisha wananchi kutembelea banda la VETA pamoja na kujiunga na Chuo hicho kilichopo Kihonda, Morogoro kwa lengo la kujifunza fani mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Post a Comment

0 Comments

TCAA YATAKA MATUMIZI YA NDEGE YAENDANE NA USALAMA WA ANGA