AUAWA NA POLISI WAKATI AKIWASHAMBULIA KWA MISHALE


 NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

MKULIMA na mkazi wa kijiji cha Chioli Kitongoji cha Manyata wilayani Chemba aliyefahamika kwa jina la Nada Songo (45), aneuawa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa na risasi maeneo ya kifuani na katika mguu wa kulia ambapo alifariki dunia wakati akiwashambulia askari wa jeshi hilo kwa mishale inayodhaniwa kuwa na sumu.

Mtuhumiwa huyo (Marehemu),akiwa na mishale inayodhaniwa kuwa na sumu alijificha kichakani nje ya nyumba yake na kuanza kurusha mishale hiyo baada ya kuwaona askari waliokwenda kumkamata.

Akizungumzia tukio hilo leo Agosti 29, 2022,jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (ACP), Martin Otieno,amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kukahidi kukamatwa na polisi kuhusianoa na kosa ambalo alilokuwa akituhumiwa nalo la kutishia kuua kwa kutumia silaha za jadi.  

Kamanda ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 27, mwaka huu baada ya marehemu kuhatarisha amani katika kitongoji hicho kwa kutumia mishale yenye sumu.

“Askari polisi walikwenda kufanya ukamataji lakini mtuhumiwa alitoroka na kukataa amri ya kukamatwa kuhusiana na makosa yake ambapo Agosti 28, mwaka huu askari polisi walipata taarifa ya kurejea kwa mtuhumiwa huku akiendelea kutishia usalama katika kitongoji hicho,” ameeleza ACP Otieno. 

Ameongeza kuwa askari hao walipokwenda kumkamkamata aliwashambulia kwa kutumia mishale inayodhaniwa kuwa na sumu na kumjeruhi askari tumboni upande wa kushoto mwenye namba H. 9377 PC William na askari wa akiba Madodo Juma ambaye amejeruhiwa kwa mshale mguu wa kulia.

Kamanda Otieno amefafanua kuwa askari polisi majeruhi amepewa rufaa ya Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa matibabu na kwamba hali yake inaendelea vizuri na askari huo wa akiba, mgambo ametibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chemba na kuruhusiwa. 

Aidha kamanda huyo ameongeza kuwa eneo la tukio limekuwa na mishale 23, visu viwili,pinde,mbili, ala ya kuwekea mishale, dawa mbalimbali za kienyeji, Hati ya kumaliza kifungo Gereza la Kingángá Wilaya ya Kondoa mfungwa namba 46/2022 kuanzia Agosti 13, 2021 hadi Februari 11, mwaka huu.

Kamanda huyo ameleleza kuwa marehemu alichimba mahandaki mawili ambayo hutumia kujificha mara afanyapo matukio ya kiuhalifu huku Kamanda huyo akisema mwili wa marehumu umefanyiwa uchunguzi na madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Chemba na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU