TFS YAPONGEZWA KWA KUKUSANYA MADUHULI BIL. 157.8 NA UHIFADHI MISITU

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana akizungimza wakati akifungua mkutano wa siku nne unaoshirikisha makamanda wa wawakilishi121wa TFS unaofanyika badala ya Baraza la Wafanyakazi ambao unatumika kama darasa kujifunza mambo mbalimbali yakiwamo ya mifuko ya hifadhi,maadili,kujadili bajeti ya mipango ya mwaka 2022 na 2023 wenye kaulimbiu ‘Tumerithi Tuwarithishe’ uliofaniyika Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku nne unaoshirikisha makamanda wa wawakilishi121wa TFS unaofanyika badala ya Baraza la Wafanyakazi ambao unatumika kama darasa kujifunza mambo mbalimbali yakiwamo ya mifuko ya hifadhi,maadili,kujadili bajeti ya mipango ya mwaka 2022 na 2023 wenye kaulimbiu ‘Tumerithi Tuwarithishe’ unaofanyika jijini Dodoma.

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA 

WZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk.Pindi Chana amewapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kwa kuongeza makusanyo ya maduhuli mwaka 2021 na 2022 ambapo walikusanya bilioni 157.8 sawa na asilimia 102.04, huku akiwataka kuendelea kuweka mikakati ya kukusanya zaidi.

Pia ameitaka TFS kuongeza ubunifu na kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazojitokeza wakati huu ikiwemo ya kuwekeza katika biashara ya kuvuna hewa ukaa.

Hayo ameyasema Jijini hapa wakati akifungua mkutano wa siku nne unaoshirikisha makamanda wa wawakilishi121wa TFS unaofanyika badala ya Baraza la Wafanyakazi ambao unatumika kama darasa kujifunza mambo mbalimbali yakiwamo ya mifuko ya hifadhi,maadili,kujadili bajeti ya mipango ya mwaka 2022 na 2023 wenye kaulimbiu ‘Tumerithi Tuwarithishe’.

Balozi Chana amewaasa wakala huo kuchangamkia fursa za miradi mbalimbali ya kimataifa itakayosaidia kuongezea raslimali fedha zitakazosaidia katika kuleta ufanisi na kuendeleza sekta hiyo ya misitu nchini.

Waziri Chana amewapongeza TFS kwa kununua vifaa vya kuboresha utendaji kazi kila mwaka, katika kipindi cha miaka miwili wamejenga nyumba mpya 62 na kununua vifaa vya ulinzi na mitambo 78, pikipiki 100 za doria, kwa kufanya hivyo kunawatia moyo makamanda na kuleta motisha katika kufanya kazi kwa ufanisi.

Pia amewaasa wasitumie silaha hizo zaidi ya kiwango kinachotakiwa badala yake watumie silaha pale inapobidi na wasizitumie kwa ajili ya kunyang’anya haki za watu.

"Mjitahidi kuzuia migogoro mipya isitokee katika maeneo mbalimbali yakiwemo ambayo Kamati Maalumu ya Mawaziri wanane ilipita na kuona migogoro," amesema.

Ameongeza kuwa maeneo ambayo tayari wavamizi wameingia, makamanda hao wakashirikiane na kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuhakikisha wanaondolewa wasiruhuru wavamie tena.

Waziri Chana alimempongeza Rais Samia Suluhu Hassam kwa kuwapandisha vyeo makamanda 479, kupanda mishahara pamoja madaraja, akawataka waendeleze juhudi kulinda raslimali misitu ambayo taifa linategemea kwa ajili ya maendeleo yake.

Naye Mkurugenzi wa Raslimali Watu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Prisca Lwangili alipongeza wakala huo kwamba katika suala la raslimali watu unafanya kazi vizuri na wameshinda tuzo kadhaa za kusimamia raslimali watu na ya mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, akawaomba waendeleze kazi hiyo nzuri ya kufanya kazi kwa weledi la uadilifu.

Kwa upande wake Kamishina wa Uhifadhi TFS, Profesa Dos Santos Silayo alimwomba waziri kukamilisha na kupata mrejesho wa ripoti ya Kamati ya Mawaziri Wanane iliyopita katika maeneo ili kumalisha changamoto ya migogoro mipaka baina ya wakala na wananchi.

Ameeleza kuwa mashamba ya miti zaidi ya 493, TFS inashughulika na nyuki na kwamba imekuwa ikitumia Sh milioni 150 kwa ajili ya kupima ubora wa asali ili kuingiza katika soko la kimataifa na tayari inauza bidhaa hiyo katika soko hilo.   

Kamishina huyo amesema wakala huyo tayari imeweka vigingi 24,000 katika kulinda hifadhi, lakini pia imekua ikitoa elimu kwa wananchi wanaozunguka na pia imesaidia vijiji 100 kupanga matumizi bora ya ardhi yake.


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA