WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUTOA MAONI


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakili Amon Mpanju, akizungumza na Wadau mbalimbali wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua Mkutano wa kupitia Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, iliyofanyika Jijini Dodoma Agosti 30, 2022.

Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuandaa Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nesia Mahenge akitoa taarifa kuhusu Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, katika mkutano wa wadau uliofanyika Jijini Dodoma Agosti 30, 2022.
Baadhi ya Wadau walioshiriki kupitia rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, wakiwa katika mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma Agosti 30, 2022.

NA ASHA MWAKYONDE,DODOMA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Malaalumu, Wakili Amon Mpanju amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na baraza la Taifa la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO), imekamilisha rasmu ya mpango mkakati wa uendelevu wa mashirika hayo.

Pia Mpanju amewataka wadau wa mashirika hayo kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni chanya yatakayosaidia kuboresha Rasimu iliyoandaliwa na kikosi Kazi cha tathmini ya maendeleo ya taarifa ya uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuwezesha utekelezaji wa Mkakati huo.

Akizungumza leo Agosti 30,2022 jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kupitisha rasimu ya mkakati wa kitaifa wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali wakili Mpanju amesema kupitia Mkakati huo, kila Shirika Lisilo la Kiserikali litaandaa Mpango Kazi wa Utekelezaji utakaowezesha taasisi za usimamizi na Mashirika yenyewe kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Ameongeza kuwa Mkakati huo unatarajiwa kuzinduliwa Rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, litakalofanyika tarehe 30 Septemba, 2022.

Akimkaribisha mgeni rasmi Wakili Mpanju, Msajili wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka Wizara hiyo Vickness Mayao amesema wameamua kutengeneza mpango makakati huo lengo likiwa ni kuyafanya mashirika hayo kuwa endelevu kwani baadhi ya mashirika yamekuwa hayafikii malengo.

Awali Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nesia Mahenge amesema kuwa katika kukamilisha tathimini ya taarifa ya uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali wamefanikiwa kutembelea kanda takribani 5 ili kuwawezesha wadau kutoka maoni kama anavyoeleza.

Mahenge ameeleza kwamba kikosi kazi hicho kimepita katika kanda zote hapa nchini kukusanya maoni yaliyosaidia kuandaa rasmu na wanaamini mpango huo ukikamilika itakuwa muarobaini kwa mashirika kujiendesha kwa tija.



Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA