PHM, WADAU WATAKA WAHUDUMU WA AFYA WAKUMBUKWE


Mratibu wa Mtandao wa Asasi za kiraia Mkoani Dodoma (NGONEDO),  Edward Mbogo ( aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.


Wadau walioshiriki mkutano wa People's Health Movement (PHM) Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika hoteli ya African Dream Jijini Dodoma.

NA MWANDISHI WETU,DODOM

MKURUGENZI Mtendaji wa Asasi ya People's Health Movement (PHM) Tanzania, Godfrey Philemon ameiomba Serikali kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya wahudumu wa Afya ya Jamii kwani wamekuwa wakiwahudumia wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini .

"Serikali inawatambua na sera ya afya inatambua mchango wao sasa ni wakati wa kuwa na mwongozo wa Kitaifa," alisema.

Akizungumza Jijini hapa wakati wa mkutano.uliowashirikisha waandishi wa Habati na asasi sizizo za Kiserikali zinazohusika na masuala ya afya alisema kuwa ni vyema Serikali ikaweka mikakati ya kuboresha maslahi ya wahudumu.hao.

Alisema kuwa sasa ni wakati wa kuwawezesha kwani ndio wataunganisha watoa huduma na waunganisha huduma katika Jamii, wataondoka tatizo la upungufu wanatoa huduma ambalo ni changamoto katika Nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Alisema kuwa baada ya mkutano huo wataenda kukutana na watoa huduma na wauguzi wa Afya ngazi ya jamii.

"Lengo nikuwatambua wahudumu wa Afya wa jamii katika maeneo yao , kwenye kamati zao Ili wawe na sauti moja.

"Tujue changamoto wanazokutana nazo katika kuhudumia kaya Ili kuwatambua wanaofanya kazi vizuri Ili wawe chachu kwa wengine," alisema.

Alitaja Nchi zilizofanya vizuri katika ngazi ya afya ya jamii ni Burkina faso, Ethiopia, Mali,Malawi, Tanzania na Uganda.

"Malawi wana siku ya Kitaifa kwa ajili ya kutambua mchango wa wahudumu wa Afya ya Jamii na Nchi nyingine zinawalipa,," alisema.

Aliiomba Serikali kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya wahudumu hao kwani wamekuwa wakifika maeneo ambayo watu wengine hawafiki

."Pongezi kwa Serikali kwa kujenga vituo vya Afya vingi, Hospitali za kanda na sasa ni wakati wa kuwa ni miuongozo inayotambua uwepo wao," alisema.

Kwa upande wake Ofisa Uelimishaji na uhusiano kutoka PHM, Tanzania Thomas Edward alisema kuwa Shirika hilo limesajiliwa kama Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ,linafanya kaci ya kuhakikisha huduma za afya kuwa haki kwa Watanzania wote,

"Kuangalia mijadala ya kusera, kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupaza sauti kwa watu wa kawaida," alisema.

Alisema kuwa kazi yao kubwa ni suala la uelimishaji,utetezi ili kila mtu apate huduma ya afya katika kiwango kizuri

"Kuangalia sera zilizopo katika masuala ya uandaaji,kufanya tathimini ya miradi iliyopo kwenye masuala ya afya, suala la udhalilishaji wa kijinsia bado ni tatizo , kuangalia zaidi wanawake wanaoonewa," alisema.

Ofisa Habari na Mahusiano wa Shirika la Alliance on Traditional Practices and Women Empowerment (ATPWE) , Mihwela Mapembe alisema kuwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wamekuwa na mchango mkubwa sana hasa maeneo ya vijijini ni vyema likafanyika jambo.kwa ajili yao.

"Tunatamani wapate utambulisho ili wawe na vitambulisho na posho ya kila mwezi kwa maana wao ndio hutambua na kuanza kushighulikia mambo mengi katika ngazi ya jamii," alisema.

Alisema kuwa wamekuwa wakiwatumia kufanya uelimishaji haswa katika kupinga ukeketaji sababu kwa sasa ukeketaji umekuja kwa njia mpya wa bibi wanawafinya au kuwasugua na madawa watoto wachanga, tumelibaini basi tunawatumia kutoa elimu Hii kwa wamama wajawazito na watoto

"Pia tunawatumia kufundisha elimu ya afya na haki za watoto mashuleni katika klabu za watoto," alisema.

Mratibu wa mtandao wa Asasi za kiraia Mkoa wa Dodoma (NGONEDO),Edward Mbogo alisema kuwa huduma bora za afya ni suala la msingi kwa kila binadamu.




Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA