WAZIRI NCHEMBA: CHIMBUKO LA TOZO NI KUUNGANISHA NGUVU KUTEKELEZA MAHITAJI YA LAZIMA


NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

SERIKALI imesema kuwa uhitaji wa bajeti kama nchi unaongezeka kwa sababu ya majukumu ya msingi kutokana na miradi mikubwa inayotekelezwa ikiwamo ya Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo bajeti yake ni Trilioni 6,hivyo suala la kodi ya tozo ni kuunganisha nguvu kutekeleza mahitaji ya lazima ambayo yalikuwa pengine yanakosa bajeti.

Pia Serikali imewataka wananchi kuwa watulivu juu ya suala la tozo huku ikiwawashukuru wananchi hao kwa kutoa maoni yao ya suala hilo la tozo na kwamba imewasikia, imepokea hivyo hivi karibuni itakuja na majibu sahihi.  

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Septema 1, 2022 wakati akitoa ufafanuzi wa awali juu ya tozo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema serikali imeweka timu ya watu kwa ajili ya kuchambua tozo hizo kwani ni lazima mtu alipe kulingana na kipato chake na sio kuwaonea wanyonge huku wenye uwezo mkubwa wa kipato wakiachwa.

Waziri Nchemba amebainisha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki na za Jumuiya ya Kiuchumi nchi za kusini mwa Afrika (SADC), hakuna nchi inyotekeleza kwa mara moja miradi mikubwa kama Tanzania.

Waziri huyo ameeleza kuwa Tanzania ina bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo ni la lazima nchi inalihitaji tangu siku nyingi, bajeti yake ni zaidi ya Trilioni 6, Reli ya kisasa hadi kukamilika inahitaji zaidi ya trilioni 23.

“Kila Mtanzania anatakiwa ajisikie farari kwa miradi mikubwa ambayo ni uti wa mgongo ambayo itageuza uchumi wa nchi yetu, Chimbuko la tozo ilikuwa ni kwa ajili ya kuunganisha nguvu kama Watanzania ili tuweze kutekeleza mahitaji ya lazima ambayo yalikuwa pengine yanakosa bajeti. ,”amesema Waziri Nchemba.

Ameongeza kuwa walianza kama mapendekezo, serikali ikapendekeza wa wakilishi wa wananchi waliona hili jambo lina mantiki walifanya kwa kuzingatia ulazima wa maeneo yenye uhitaji wa ulazima.

Waziri Nchemba ameyataja maeneo hayo kuwa ni madarasa, kujenga vituo vya afya, Ununuzi wa vifaa, nyumba za walimu, ujenzi wa miundombinu huku akileza kuwa kabla ya mwaka mmoja uliopita ikilinganishwa na kule nyuma kuna tofauti kubwa barabara zilikuwa hazipitiki hata kidogo lakini sasa zinapitika.

Amesema kuwa wanawekeza nguvu kwenye shughuli za kiuchumi kwani vijana wengi hawana ajira na wale wenye kipato kidogo wapo wengi hivyo serikali kupeleka nguvu kazi ya vijana hao waingie kazini huku akieleza kuwa kwa sasa wahitimu wanawategemea wastaafu.

Naye Waziri, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa ameeleza kuwa tayari serikali imejenga vituo vya afya 234 ndani ya mwaka mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 117 na bilioni 149.5 zilitumika kwa ajili ya manunuzi ya vifaa kupitia tozo za mialamala ya simu.  

‘’Tozo hakika zimekuwa ni mwarobani katika kuboresha miundombinu pasipo kuwapo na vituo vya afya karibu kuna gharama kubwa kwa wananchi, naishukuru serikali kwa kuwezesha miamala ya tozo kupitia simu,’’ amesema Waziri Bashungwa.



 

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA