IDADI YA WATALII NCHINI YAONGEZEKA NA KUFIKIA ASILIMIA 62.7


 NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema kuwa idadi ya watalii walioingia nchini kuanzia Januari hadi Julai yaongezeka hadi kufikia 742,133 ikilinganishwa na 456,266 kwa kipindi Cha mwaka 2021, sawa na asilimia 62.7.

Kutokana na umuhimu wa sekta ya Utalii katika kuingiza fedha za kigeni nchini taasisi zinazotoa huduma kwa watalii zina wajibu wa kuendelea kuboresha zaidi huduma hizo kwa lengo kuvutia watalii wapya na wanaokuja nchini kwa mara nyingine.

Hayo yamesemwa leo Agosti 17,2022 na Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi kutoka NBS, Daniel Masolwa wakati  akitoa taarifa ya mwenendo wa watalii walioingia nchini amesema kati ya watalii hao 742,133 walioingia nchini 222,449 waliingia kupitia Zanzibar sawa na asilimia 30.0 ya watalii wote.

Amefafanua kuwa watalii walioingia nchini Julai 2022 pekee waliongezeka hadi 166,736 ikilinganishwa na watalii hao 81,307 walioingia Julai 2021 sawa na ongezeko la asilimia 105.1.

" Idadi ya watalii walioongezeka mwezi Julai 2022 ilikuwa zaidi ya mara mbili ya watalii walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021, " ameeleza Mkurugenzi huyo.

Masolwa amebainisha kuwa idadi kubwa ya watalii walioingia nchini kutoka nchi zilizo nje ya Bara la Afrika katika kipindi cha Januari hadi Julai 2022 walitoka Marekani ikiwa na watalii 51.301.

Amezitaka nchi nyingine kuwa ni Ufaransa 47,403, Ujerumani 30,817, Poland 29,004 na Uingereza 28,275 na kwamba katika mwezi Julai 2022 idadi kubwa ya watalii walioingia nchini walitoka Marekani 17,135, Ufaransa 12,634, Uingereza 8,586, Ujerumani 8,015 na Netherland 5,102.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Tanzania ilipokea  watalii kutoka Bara la Afrika katika kipindi cha Januari hadi Julai idadi kubwa ya watalii walitoka Kenya 86,220, Burundi 54,877,Malawi 27,079, Uganda 21,080 na Afrika Kusini 20,868.

Pia Masolwa amesema katika kipindi cha mwezi Julai 2022 idadi kubwa ya watalii walioingia nchini walitoka Kenya 16,654, Burundi 7,966, Malawi 5,113, Afrika Kusini 4,335 na Rwanda 4,035.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI