BRELA yashauriwa kuwasaidia wafanyabiashara mkoani Mara

Rais wa TCCIA Bw Paul Koy akiongea na maafisa kutoka Wakala was Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) alipotembelea alipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Biashara ya Mara International Business Expo 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Mukendo katika mji wa Musoma, mkoani Mara.

Rais wa TCCIA Bw Paul Koy akisalimiana na Afisa Sheria wa BRELA Bi Neema Nyadzi alipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Biashara ya Mara International Business Expo 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Mukendo katika mji wa Musoma, mkoani Mara.

NA MWANDISHI WETU 

RAIS wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Bw. Paul Koy ameishauri Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kusaidia wafanyabiashara wa mkoa wa Mara ili warasimishe biashara zao. 

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 4 Septemba, 2022 alipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Mara Business Expo 2022 yanayofanyika Musoma, mkoani wa Mara.

"Nawaomba sana BRELA muwasaidie wafanyabiashara wa mkoa huu maana wanahitaji sana huduma zenu", ameeleza Bw. Koy.

Bw. Koy amesisitiza kuwa mbali na kutoa huduma za usajili na utoaji wa leseni kwenye banda inabidi BRELA itoe elimu kwa wananchi wanaozalisha bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake Afisa Leseni wa BRELA, Bw. Rajab Chambega amemhakikishia kuwa Taasisi hiyo imejipanga vema kutoa huduma kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara na mikoa jirani wanaotembelea maonesho hayo.

Pia ameeleza kuwa kila mfanyabiashara anayeshiriki maonesho hayo atatembelewa na kupewa ushauri na pia kusaidiwa kurasimisha biashara yake.

BRELA inashiriki kwenye Maonesho ya Mara Business Expo 2022 na kutoa huduma za usajili na utoaji wa leseni papo kwa hapo hadi tarehe 11 Septemba, 2022.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI