LICHA ya Serikali kuendelea kuboresha mfumo wa utoaji elimu kwa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora imeelezwa kuwa zipo changamoto zinazo kwamisha programu ya elimu jumuishi inayowawezesha watoto wenye ulemavu kupata elimu kama watoto wengine ambao hawana ulemavu.
Akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Majadiliano juu ya Elimu Jumuishi wa kuboresha Mazingira Salama ya Jumuishi Kwa Watoto wote Tanzania,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la child support Tanzania Noela Msuya amebainisha changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu kupata elimu kuwa ni kukosekana kwa mfumo wa kupima vipaji kwa watoto, uhaba wa walimu na wataalamu wa elimu jumuishi na vifaa saidizi.
Amesema kuwa lengo lao ni kukuza uelewa na kuhakikisha wanapata elimu bora katika mfumo wa elimu jumuishi.
" Child support Tanzania tunaamini katika mambo manne usawa kwa watu wote lakini pia tuna amini ulemavu sio kushindwa, tuna amini katika utaendaji wa kijamii kazi zetu zote tunaamini inapohusishwa zinaweza kwenda vizuri zaidi na kuwa na mwendelezo pamoja na kuthamini vipawa, vipaji kwa watoto wenye ulemavu," amesema Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa tangu wameanza kazi zao miaka 14 iliyopia wameweza kuwafikia watoto zaidi ya 1000 wenye mahitaji maalamu ambapo wamehakikisha wamewapeleka shuleni na wale ambao walikuwa shuleni wamehakikisha wamepandishwa madaraja.
Akifungua mkutano huo Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa elimu jumuishi itasaidia kuwawezesha watoto wenye ulemavu kupata elimu itakayowasaidia kupiga hatua ya kuondokana na ujinga na umasikini huku akibainisha juhudi zilizofanya na serikali hadi sasa.
Dk.Tulia ameeleza kuwa watashirikiana na shirika hili pamoja na serikali kuhakikisha elimu Jumuishi inapewa kipaumbele.
" Nitoe wito kwa Taasisi na mashirika mbalimbali kujifunza kutoka Kwa Shirika la Child support Tanzania nafurahi kuona wapo tayari kutoa uzoefu wao katika kuhakikisha jamii zetu zinakuwa bora zaidi kuliko ilivyosasa kwa maana ya kutoa elimu hii jumuishi," amesema Dk. Tulia.
Akizungumza kwaniaba ya washiriki wa mkutano huo mwenyekiti wa chama cha viziwi, na wasioona David Shaba ameitaka serikali kuwajali wenye ulemavu kwa
kuhakikisha wanapata elimu sambamba na kutenga bajeti ya kufadhili wenye ulemavu kwa fedha za ndani badala yakutegemea wafadhili kutoka nje.
" Naomba ulivalie njuga suala hili la watu wenye ulemavu kupata elimu kuna umuhimu mkubwa wa kutegewa bajeti kwa sababu miradi mingi inakwama kwa kukosa ufadhili na hatuwezi kutegemea wafadhili kutoka nje ya nchi wakati rasilimali zote tunazo," amesema.
Aidha mwenyekiti huyo ameomba watu wenye ulilemavu kutengewa bajeti maalumu ya watu hao
Huku akimshukuru Dk. Tulia kwa kutambua elimu Jumuishi haitapata mafanikio kama mahitaji maalamu hayatazingatiwa.
Child support Tanzania imekuja na program ya 'Peleka Rafiki Zangu Wote Shuleni' yenye lengo la kuhakikisha watoto wote wanaenda shule pamoja na kuwafichua waliofichwa majumbani.
kwa wenye mahitaji maalamu.
0 Comments