HANJE AZINDUA PROGRAM YA 'VIJANA MAKINI'


 Mbunge Kijana wa Viti maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Nusrath Hanje akizungimza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua program ya 'Vijana Makini'


Mkurugenzi Mtendaji wa TYVA Yusufu Bwango akizungumza na washiriki vijana waliohudhuria uzinduzi wa program ya 'Vijana Makini'

Mkurugenzi Msaidizi Uratibu na Uwezeshaji Kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Eliakm Mtawa akielezea jambo Kwa washiriki wa uzinduzi wa program ya Vijana Makini'.

Baadhi ya washiriki vijana waliohudhuria uzinduzi wa program ya 'Vijana Makini'.

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

MBUNGE Kijana wa Viti maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Nusrath Hanje amesema vijana wanatakiwa wajitambue, nguvu waliyonayo kitaifa kwa kuwa hata watu wakitaka kufanya maandamano wanawategemea wao. 

Pia amesema wao kama vijana wanasubiri Oktoba Rais Samia Suluhu Hassan atangaze matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo imefanyika Agosti 23, mwaka huu huku akisema idadi itawasaidia wao kama watetezi, wakilishi wa vijana kupata nguvu ya kuongea kwa kuwa Sensa hiyo itawaonyesha idadi kubwa ya Watanzania ni vijana.

Hayo ameyasema juzi wakati akizibdua program ya 'Vijana Makini' inayoendeshwa na Shirika linalofanya kazi za Utetezi, Ushawishi na Masuala mbalimbali ya Vijana (TYVA), amesema kuna nafasi ya vijana kwa serikali ambayo inatengezeza mbinu wezeshi kwa vijana hao kuwafanya wawe na uwezo wa kujitambau katika nyanja mbalimbali ikiwamo Kiuchumi.

" Sisi kama vijana tunasubiri matokeo ya Sensa atakayoyatangaza Rais Samia ndicho kitakachosema na kutusaidia sisi wabunge vijana bungeni, vijana wa TYVA wanafanya kwa nafasi yao sehemu kubwa ya vijana na program hii itachukua mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2024 hivyo TYVA wajibu wao ni kutoa taarifa kutupatia niwapangeze," amesema Hanje.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TYVA Yusufu Bwango amewashauri vijana hao wajiunge kwa wingi katika shirika hilo ili kutoa taarifa za changamoto zao zinazowakabili.

Amesema miongoni mwa changamoto ambazo zinawakuta vijana hao ni ukosefu wa kupata taarifa, kuzitafuta huku akisema program hiyo inaawasaidia vijana hao kujua mambo mengi yakiwamo suala la bajeti.

" Vijana wajiunge katika vikundi kazi kwa lengo la kuibua changamoto zao ambazo kama wanaona kupitia serikali za mitaa ni ngumu kufanikiwa bila kujali kada zao za kisasa,dini na rangi wajiunge ili waweze kutoa changamoto zao," ameeleza Mkurugenzi huyo.

Awali Mkurugenzi Msaidizi Uratibu na Uwezeshaji Kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Eliakm Mtawa ameeleza kuwa kuna mabadiliko mengi ya kiuwezeshaji kiuchumi kwa vijana yakiwamo masuala ya uwezeshaji katika stadi za maisha.

Program hiyo ya 'Vijana Makini' ina lengo la kuhakikisha vijana wanakuwa na ushirika madhubuti katika ushawishi na utetezi wa masuala ya vijana kwenye mchakato wa bajeti ya serikali.






Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI