WAZIRI UMMY: WAGONJWA 54 WATHIBITIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA SURUA


 NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imesema jumla ya wagonjwa wote  54 wamethibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Surua kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti mwaka huu hapa nchini na hakuna kifo kilichotolewa taarifa kutokana na ugonjwa huo.

Pia imesema kumeonekana ongezeko la wagonjwa watu wenye dalili za homa na vipele 38  ambao ni wahisiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya waliothibitika katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Agosti mwaka huu. 

Hayo yamesemwa leo  jijini hapa  na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu ongezeko la wagonjwa wa Surua nchini alisema uchambuzi wa majibu ya vipimo kutoka Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kwa sampuli za Julai hadi Agosti umeonyesha kuwa Halmashuri saba zimekidhi vigezo vya kuwa na kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Surua ambapo wagonjwa 38 wakithibitika katika Halmashuri hizo.

Waziri huyo alizitaja Halmashuri hizo kuwa ni Bukoba sampuli tatu, Handeni DC nne, Kilindi sampuli tatu, Mkuranga Nne, Manispaa ya Kigamboni babe,Manispaa ya Temeke  kumi na mbili  na Manispaa ya Ilala  nne.

Alifafanua kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Surua huthibitika pale ambapo sampuli tano za wahisiwa  kuchukuliwa kutoka katika Wilaya moja ndani ya mwezi mmoja na endapo sampuli hizo tatu au zaidi kati ya tano zilizochukuliwa zimetoa majibu chanya.

Waziri huyo alieleza  uchambuzi huo pia ulionesha uwepo wa wagonjwa hao katika Halmashuri za Arusha moja, Chalinze mbili,Igunga moja,Kahama MC moja, Kalambo moja, Kigoma DC mbili, Kwimba DC moja, Masasi Tc moja, Mvomero DC mbili Rorya DC mbili, na Manispaa ya Ubungo mbili huku alifafanua kwamba Halmashuri hizo hazikukizi vigezo vya kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Surua.

" Hakuna kilichotolewa taarifa kutokana na ugonjwa huu, kati ya wagonjwa Hawa 54 waliothibitika wagonjwa 48 walikuwa na umri usiozidi miaka 15 na wagonjwa 6 walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 15," alisema Waziri Ummy.

MIKAKATI YA WIZARA

Waziri huyo aliongeza kuwa katika kudhibiti ugonjwa huo Wizara hiyo inaendelea kuchukua hatua mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukmarisha ufautiliaji wa wahisiwa kupitia mfumo wa ufautiliaji wa magonjwa na tetezi katika ngazi ya jamii.

Alieleza kuwa Wizara hiyo itatuma timu kwenda katika maeneo yaliyoathirika na kwa kuwa na wagonjwa wengi  pamoja na kutoa elimu kwa watoa huduma za afya na jamii kuhusu dalili na jinsi ya kujikinga  na ugonjwa huo.

DALILI

Akizungumzia dalili za ugonjwa huo Waziri Ummy alisema homa na vipele inayoweza kuambatana na kikohozi mafua, macho kuwa mekundu na vidonda mdomoni.

" Ugonjwa huu hauna tiba maalumu bali matibabu hutolewa kulingana na dalili zinazojitokeza. Ugonjwa huu usipodhibiwa mapema huweza kuleta madhara katika masikio au kusababisha homa ya mapafu, upofu wa macho homa ya uti wa mgongo  na kusababisha kupoteza maisha," alisema.

Akizungumzia kuhusu chanjo aliitaka jamii kuwapeleka watoto kwenye chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wapatiwe chanjo ya Surua, Rubella kulingana na umri.

Aidha Waziri Ummy aliwataka Waganga  Wakuu wa mikoa na Halmashuri zote nchini kuchukua hatua katika kudhibiti ugonjwa huo. 

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU