MWANAFUNZI WA NIT AJA NA TEKNOLOJIA YA KUUZA MAZIWA KIDIGITALI




Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Elizabeth Massawe akiwaekezea  teknolojia ya ukuzaji wa maziwa kidigitali watu waliotembelea banda la chuo hicho.

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

MWANAFUNZI wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Elizabeth Massawe amebuni mashine ya  'Automatic Milk Vending' ambayo inatumia mfumo wa kidigitali kuuza maziwa na kumrahisishia mfanyabiashara kupunguza gharama za kuajiri na badala yake  atakuwa anangalia kwa kutumia mfumo huo  kujua wateja wangapi walionunua maziwa na amepata kiasi gani kwa siku.

Ameomba serikali kuchukua muda wa kutathimini bunifu mbalimbali zinazobuniwa na wanafunzi wa vyuo ili kuziendsleza na kuweza kutoa ajira kwa vijana wengi wakitanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na   Taifa kwa ujumla.

Akizungumza leo Septemba 22,2022, kwenye maonesho ya maadhimisho ya Siku ya wahandisi jijini hapo katika banda la NIT, Elizabeth amesema kuwa mashine hiyo  inafanya kazi kwa kutumia mfumo wa kidigitali ambapo mfanyabiashara atakaa nyumbani huku biashara yake ya maziwa inaendelea kama kawaida.

Mwanafunzi huyo ameeleza kuwa mteja atakapohitaji maziwa ataweka kiasi cha fedha na atapata maziwa kulingana na hela yake huku akitolea mfano mteja huyo akiweka shilingi 100 atapata maziwa milimita  300 na taarifa itamfikia mmiliki kupitia web site yake.

Amesema lengo la kubuni teknolojia hiyo ili kumsaidia mfanyabiashara asitumie mikono na muda mwingi kufanya biashara hiyo kama kusafisha kila dakika katika eneo lake la biashara na ukusanyaji wa hela. 

"Mmiliki wa hii mashine atakuwa anajaza maziwa pale yatakapokuwa yameisha na kuendelea na shughuli nyingine  na atajua kupitia mfumo wateja wangapi wamenuna maziwa na kiwango cha fedha kinaonekana,  tarehe  na muda wa mteja alionunua maziwa," amesema mwanafunzi huyo.

Amefafanua kuwa kupitia mashine hiyo mmiliki atajua ameuza kiasi gani na wateja wangapi waliofika kununua maziwa na glasi ngapi kwa siku ameuza.

Elizabeth amesema hadi kukamilika kutengeneza mashine hiyo imechukua muda wa miezi miwili na  gharama za malighafi ni  shilingi 180,000.

Akizungumzia changamoto katika utengeneza wa mashine hiyo Elizabeth amesema kuungua kwa vifaa mara kwa mara hali iliyomsababishia kufikisha muda huo.

Akizungumzia teknolojia hiyo Mkazi wa Makulu aliyetembelea banda hilo Jonathan Alex ameitaka jamii kuondoa dhana ya kwamba mwanamke hawezi kufanya jambo kubwa ambalo linaweza kufanywa na mwanaume.

"Huyo ni binti amejitahidi sana kutengeneza teknolojia hii ameangalia mbali sana, dunia ya sasa hivi ni ya sayansi na teknolojia hivyo serikali iwapatatie kipaumbele wabunifu kama hawa hasa wanawake," amesema Mkazi huyo.

Kwa upande wake Mkufunzi Uhandisi wa Matengenezo ya ndege kutoka NIT, Castory  Njako amesema kuwa miongo mwa bunifu  zilizofanya vizuri chuoni hapo na baadae zikashindanishwa wakati wa maonesho ya Siku ya wahandisi wanawake bunifu hizo zilishinda.

 Aidha amewakaribisha wananchi wa Dodoma kwenda kuona fani za uhandisi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho huku akiwahamasisha vijana kujiunga.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI