NIT YAJA NA MASHINE YA KUOSHA GARI KWA KUTUMIA DAKIKA 3


 Mwanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),katika kozi ya uhandishi wa Mitambo, Helen John akielezea 'Automatic Car Washing Machine hiyo inavyofanya kazi.

NA ASHA MWAKYONDE,DODOMA

MBUNIFU na mwanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),katika kozi ya uhandishi wa Mitambo, Helen John amebuni mashine ya  kuosha gari 'Automatic Car Washing Machine' ambayo ina  hatua  tano katika ufangaji kazi wake wa KUOSHA hadi kukamilika ambapo  inatumia dakika 3 na sekunde 49 hadi gari hilo kukamilika. 

Akizungumza leo Septemba 22,2022, kwenye maonesho ya maadhimisho ya Siku ya wahandisi jijini hapo katika banda la NIT, Heleni  amesema lengo la kubuni  mashine hiyo ni kutunza muda pamoja na kupunguza matumizi mengi ya maji huku akisema kwa sasa magari yamekuwa mengi mtu anapeleka gari kuosha anakaa zaidi ya saa mbili akisubiria foleni yake.

Amefafanua kuwa hatua hizo tano katika uoshaji gari ni kwamba  kuna kifaa cha maji masafi, sabuni, brashi la kusafishia gari, maji ya kulisuuza na baadae kukausha hatua hizo  zikikamilika gari hiyo itakuwa imeshatakata na kukaushwa.

Amesema mfumo huo unatunza muda zaidi na kwamba kwa siku mtu anaweza kuosha magari mengi zaidi ikilinganishwa na wale waosha kwa kutumia mikono hivyo  mashine hiyo inatumia dakika 3 na sekunde 49.

"Kwa kawaida gari inaoshwa dakika 15 na  zaidi lakini kwa kutumia mashine hii kwanza ina okoa muda pia mmiliki hatatumia nguvu kuosha gari kwani mashine ndiyo itafanya kazi sio mikono," amesema Helen.

Helen ametoa wito kwa serikali kuziendeleza  bunifu zao kwa kuwa dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia hivyo suala la utunzaji muda ni la muhimu katika maendeleo.

Kwa upande wake Mkufunzi Uhandisi wa Matengenezo ya ndege kutoka NIT, Castory  Njako amesema kuwa miongo mwa bunifu  zilizofanya vizuri chuoni hapo na baadae zikashindanishwa wakati wa maonesho ya Siku ya wahandisi wanawake bunifu hizo zilishinda.

Aidha amewakaribisha wananchi wa Dodoma kwenda kuona fani za uhandisi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho huku akiwahamasisha vijana kujiunga.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU