Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Akizungumza jijini hapa leo Septemba 22,2022 wakati wa ufunguzi maadhimisho ya Siku ya 19 ya Wahandisi,.
Jumla ya ahandisi zaidi ya 200 wakika kiapo cha maadili katika madhimisho ya Siku ya 19 ya Wahandisi.
NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA
SERIKALI imesema idadi ya wahandisi nchini bado ni ndogo kulingana na mahitaji halisi ambapo walipo ni
sasa ni 33,773 , Kati ya idadi hiyo, Wahandisi 30,921 ni watanzania na Wahandisi 2,852 ni wageni.
Pia serikali imeiomba Bodi ya Wahandisi kuendelea na juhudi zake za kuwaendeleza wahandisi wanawake, ambapo kwa sasa waliopo 4,012 sawa na asilimia 12.98 kimsingi idadi hiyo bado ni ndogo.
Akizungumzi jijini Dodoma leo Septemba 22,2022 wakati wa ufunguzi maadhimisho ya Siku ya 19 ya Wahandisi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameeleza kuwa ni ukweli usiopingika kwamba idadi hiyo babo ni ndogo kulingana na mahitaji halisi.
Prof. Mbarawa amesema kuwa idadi hiyo ya Wahandisi wanawake ni ndogo hivyo ni vema Bodi hiyo inaendelea na juhudi zake ikiwemo kuwatafutia nafasi za kuongeza uwezo (training opportunities), ili waweze kusajiliwa kwa wingi zaidi baada ya kuhitimu masomo yao ya uhandisi vyuoni.
Ameongeza kuwa nia isiwe tu kuleta usawa wa kijinsia kama ilivyoainishwa katika lengo namba 5 la SDGs, bali kuleta amani na usalama duniani kwa mujibu wa Tamko la Umoja wa Mataifa la mwaka 2015.
Prof. Mbarawa amebainisha kuwa serikali itaendelea kuongeza na kuimarisha vyuo vyetu vinavyofundisha wahandisi na kupitia Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kusomesha wataalamu hawa kwa kiwango cha Stashahada (Diploma) na Digrii.
"Nachukua fursa hii kuwapongeza Wizara na Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa juhudi zenu za kuendeleza wahandisi wahitimu (ambao kama alivyosema Msajili wa Bodi idadi yao ni takribani 3,500 kwa mwaka); kupitia mpango wa Structured Engineers Apprenticeship Programme (SEAP). Mpango huu unahitaji fedha nyingi na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mafunzo haya," amesema.
Aidha amesema serikali itahakikisha sheria ya local content inazingatiwa ili kuwawezesha wahandisi wazawa waweze kushiriki kikamilifu hasa katika miradi mikubwa.
Prof. Mbarawa ameeleza kuwa serikali inaendelea kutekeleza miradi mingi katika nchi ambayo ni Ujenzi wa Miundombinu katika sekta mbalimbali za reli, barabara, umeme, maji, viwanda, madini huku akisema watekelezaji wakuu wa miradi hiyo ni wahandisi hao.
"Nichukue fursa hii pia kuipongeza Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) na Menejimenti pamoja na Sekretarieti yote kwa kuandaa mkutano huu mkubwa na muhimu wa Sekta ya Uhandisi nchini," amesema Prof. Mbarawa.
Aidha amewapongeza Wahandisi wote wa Tanzania kwa maadhimisho hayo kwa mara ya 19 tangu 2003 pamoja na kutwataka wahandisi hao kuwa na weledi na umakini katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba kikubwa zaidi ni uwajibikaji kwa umma kudumisha maadili na kukumbuka viapo vyao.
Akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi, Mhandisi Aisha Amour amesema Wizara imekuwa ikitoa msisitizo kwa wahandisi kufanya kazi kwa uweledi na ubunifu wa hali ya juu na kuachana dhana ya kufanya kazi kwa mazoea huku akisema watakaokwenda kinyume wachukuliwa hatua kwa watakao kiuka maadili.
Pia ameongeza kuwa Wizara inaendelea kupitia kanuni za sheria na viwango vinavyotumika katika kazi za kiuhandisi huku akisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa Bodi ya wahandisi na yale yatakayo jadiliwa katika mkutano huo yanafanyia kazi kwa wakati na Taarifa ya utekelezaji itatolewa katika mkutano unaofuata.
" Wizara inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha vijana wanapata mafunzo ya kiutalaamu," amesema.
Awali Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Bernard Kavishe amesema kuwa Bodi itawaapusha wahandisi wataalamu ambao wamesajiliwa kwa mujibu wa sheria hivyo jumla ya wahandisi zaidi ya 200 watakula kiapo cha maadili.
Katika maadhimisho hayo ya 19 ya Siku ya wahandisi, wameapisha pamoja na kuzawadiwa wahandisi 36 ambao wamefanya vizuri 10 wakiwa ni wakike.
0 Comments