WAFAHAMU WANAFUNZI BORA WA NIT 2021

Mhitimu wa kozi ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege 
Peter Peter Killabuko (kulia), na 
Mhitimu wa kozi  ya Uhandisi wa Mitambo Ibrahim Korwelio wakiwa na vyeti vyao katika banda  la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

WAHITIMU  wa Chuo cha Taifa  Usafirishaji (NIT), ambao ni wanafunzi bora wa mwaka 2021 katika masomo ya Uhandisi wa  Matengenezo ya ndege na Uhandisi wa Mitambo wamezawadiwa kompyuta mapakato, midali, vyeti na fedha taslimu 500,000 kila mmoja katika maadhimisho ya siku ya Wahandisi ambayo imeenda sambamba na maonesho.

Wakizungumza jijini hapa jana kwenye banda la NIT katika maadhimisho ya Siku ya Wahandisi mara baada ya kukabidhiwa zawadi hizo wamesema lazima vijana waweke dhamira kubwa katika masomo hayo lengo likiwa ni kuja kutatua matatizo ambao yaikabilia jamii iliyowazunguka na nchi kwa ujumla.

Peter Peter Killabuko  ambaye amehitimu katika kozi ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege amewataka vijana wenzake waliopo vyuoni kusoma kwa bidii na kujifunza hasa katika kozi hiyo.

Mhitimu huyo ameeleza kuwa katika jamii kuna matatizo mengi watu wa kuyatatua ni vijana wasomi ambao wanasoma masuala ya uhandisi ambayo wanajifunzi katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kikiwamo cha NIT.

Amefafanua kuwa nchi ina uhitaji wa wasomi kama wao hivyo wanafunzi waliopo vyuoni wawe makini kujifunza pamoja na kuwasikiliza walimu wao.

"Leo  (Jana),tumezawadiwa na ERB zawadi za wanafunzi bora katika fani mbalimbali za uhandisi mimi nikiwa nawakilisha Chuo Changu cha NIT katika fani ya Uhandisi wa Matengenezo ya ndege nina furaha kubwa kwa siku ya leo kwa sababu nimekabidhiwa zawadi hizi za midali, laptop na fedha taslimu laki tano na cheti cha utambulisho wa mwanafunzi bora wa matengenezo ya ndege, " amesema.

Kwa upande wake Mhitimu wa kozi  ya Uhandisi wa Mitambo Ibrahim Korwelio  amesema amekuwa mwanafunzi bora wa Uhandisi wa mimbo mwaka 2021.

Akizungumzia fani ya Uhandisi wa Mitambo amesema ni nzuri kwa kuwa fani hiyo ni fani mama katika uhandisi na kwamba masomo yake sio magumu lakini  inahitaji mtu kujitoa na kuwekeza akili nyingi kwenye masomo hayo.

" Mimi kama Mhandisi wa Mitambo katika sayansi na teknolojia inapo kwenda tofauti na awali tulipotoka wahandisi walikuwa wakitumia vyuma hivyo laptop hii nitaenda kutumia katika kazi za uhandisi," amesema.

Ameiomba serikali kuangalia bunifu za wanafunzi kuanzia shule za mising hadi vyuoni kwa lengo la kuwa na uelewa mpana zaidi na kujitanbua.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU