PROF. MAKAME ATARAJIWA KUWA MGENI RASMI WIKI YA WAHANDISI


 NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

WAHANDISI 3500 kutoka ndani na nje ya nchi ambazo ni Kenya, Uganda na Zambia wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya wiki ya wahandisi inayoanza kesho jijini hapa kwa lengo la kubadilisha uzoefu ambapo kutakuwa na mabandda zaidi ya 80 ya maonesho  ambayo ni ya kiteknolojia ya kisasa.

Akizungumza jijini hapa Septemba 
 21,2022, na waandishi wa habari  Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Bernard Kavishe amesema katika wiki hiyo wataonesha teknolojia ya kisasa  pamoja na kujifunza, kubadilisha uzoefu na kufahamiana na kwamba kuna kampuni zaidi 134 za nje zinafanya kazi nchini.

Msajili  huyo ameeleza katika mabanda hayo bidhaa zitakazo oneshwa zinaendana na masuala ya uhandishi hivyo itakuwa ni sehemu ya kujifunza na kujitangaza huku akisema siku ya ufunguzi wanatarajia kupokea hotuba kutoka kwa viongozi wao pamoja na maelekezo.

Ameeleza kuwa Bodi hiyo itaeleza wanafanya nini pamoja na kutoa maelekezo kwa watu wanaowasimamia na kwamba kutakuwa na  bidhaa za kitaaluma ambazo zitaoneshwa za teknojia mpya hasa katika miradi ya kimkakati.

" Ni muda mzuri wa wadau wa sekta ya uhandishi kujinoa upya na kujua sekta hii inauelekeo gani," amesema Msajili huyo wa Bodi.
 
Msajili huyo wa Bodi ameeleza kuwa wiki hiyo itatumia fursa kuwaleta kundini wahandisi wapya pamoja na kuwaapisha wahandisi hao zaidi ya 400 huku akieleza kiapo hicho kinasisitiza kuweka mbele maslahi ya Umma.

"Mwaka huu tena tuna maadhimisho ya siku ya wahandisi ambayo inafanyika Dodoma katika ukumbi wa Jakaya kikwete kuanzia kesho Septemba 22 Hadi 23 siku ya kesho ni ya ufunguzi maadhimisho shughuli zitaanza mgeni rasmi tunatarajia awe Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa Makame,"amesema.

Mhandisi Kavishe amesema shughuli za awali zimeshaanza leo na washiriki wanapokea  vifaa vya mkutano na kujiweka sawa na mkutano huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi  ya maadhimisho ya wiki hiyo Mhandisi,Benedict  Mukama ameeleza kuwa mkutano huyo utakuwa mubashara ntandaoni na tayari watu zaidi ya 800 wameshajisali kwa njia ya mtandao.



Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI