MRADI WA UBORESHAJI AFYA YA MIMEA WAZINDULIWA NCHINI


Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

MWAKILISHI wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU),Cedric Merel,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini  katika hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu  ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma ,akitoa salamu za Kamati yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini katika hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi  Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania  T( Dk. Efrem Njau,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini katika
 hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.


Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Nyebenyi Tipo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini katika hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde (hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini katika hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Picha zote kwa hisani ya Full Shangwe Blog

NA ASHA MWAKYONDE,DODOMA

MRADI wa Uboreshaji  wa Huduma za Afya ya Mimea Tanzania kwa Usalama wa Chakula wazinduliwa ambao  unalengo kusaidia kudhibiti visumbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayoingia ,kutoka hapa nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango vya kimataifa katika masoko.

Serikali  ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani (FAO) na Umoja wa Ulaya (EU),
umezindua  lengo likiwa ni kuhakikisha usalama wa Chakula na kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa utoaji wa usafi wa Mazao yanayoingia na kutoka  nchini.

Hayo yamesemwa jijini hapa  leo Septemba 21,2022 , na Naibu Waziri wa Kilimo  Anthony Mavunde wakati akizindua mradi huo  amesema umetokana na ukaguzi uliofanyika  nchini mwaka 2017 katika mifumo maalumu ya udhibiti wa mimea na mazao yanayosafirishwa kwenda nchi za jumuiya ya Ulaya na ukaguzi huo kubaini mapungufu ya afya ya mimea.

“Niwashukuru EU na FAO kwa kufadhili mradi huu muhimu ni imani yetu kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa na hivyo kuongeza upatikanaji wa masoko ya kimataifa na kuchochea uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja” ameeleza.

Aidha Mavunde ametaja baadhi ya maeneo yaliyobainika kuwa na mapungufu hadi kupelekea kuanzishwa kwa mradi huo ni maarifa madogo kwa wakaguzi kuhusu matakwa ya usafi wa mazao hayo,  kukosekana kwa mfumo kukusanya takwimu za visumbufu vya mimea, kukosekana kwa maabara zenye uwezo wa kufanya uchunguzi muhimu ili kuthibiti cheti cha usafi wa mimea.

“kufuatia kubainika kwa mapungufu hayo na gharama za kufanya biashara ya mazao kuwa juu serikali ilichukua hatua kwa kuunganisha majukumu ya TPRI na ya afya ya mimea na viwatilifu TPHPA ambacho kimekuwa ni chombo kinachotambilika kimataifa” ameeleza Mavunde.

Hata hivyo ameeleza kuwa  kuja kwa mradi huu utawezesha kufikia malengo ya kuhakikisha ukuaji wa sekta ya kilimo hapa nchini kwa asilimia 10 na mauzo ya mazao ya kilimo yanaongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.2 za sasa hadi kufikia Dola bilioni 5 ifikapo mwaka 2030.

Amebainisha kuwa  Wizara ya Kilimo itasimamia utaratibu na kuongeza utekelezaji wa mradi huo na kutaka kamati ya kusimamia mradi huo na kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kuwasimamia wataalamu ili kazi zilizopangwa kwenye mradi zitekelezeke kwa wakati.

Awali Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo  Obadia Nyagilo amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mika mitatu na nusu kwa kiasi cha Euro milioni 10.1 kwa ushirikiano ambapo Jumuiya ya umoja wa Ulaya itatoa Euro milioni 9.5, FAO itatoa Euro 350’000 na Tanzania itatoa EURO 250,000.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na  Uthibiti wa Viuatilifu Tanzania  (TPHPA) ,Dk.Efrem Njau amesema sekta ya kilimo ni muhimu sana ambapo imeajiri zaidi ya asilimia 67 ya watanzania na kuchangia takribani asilimia 29 ya pato la taifa.

Dk. Njau ametaja baadhi ya majukumu yanayofanywa na mamlakae hiyo kuwa ni kusimamia na kuratibu tasnia nzima ya viuatilifu, kudhibiti ubora, uagizaji, usambazaji na kuchagiza matumizi sahihi na usalama wa viuatilifu, kufanya uchambuzi wa athari ya visumbufu.

"Matokeo tarajiwa ya mradi huo ni kuziongezea uwezo maabara za mamlaka kujenga, kukarabati na kuweka vifaa katika maabara za Mamlaka, kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa visumbufu na masalia ya viuatilifu katika mnyroro wa thamani ya uzalishaji wa mazao hususa ni yale mbogamboga na matunda” amesema.

Ameongeza kuwa mradi huo  utakuwa na kamati ambayo itaundwa na itawajibika kukutana na mara mbili kwa mwaka kupitia na kuhakikisha malengo ya mradi yanakwenda kama yalivyopangwa.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO),Nyebenyi Tipo amesema mradi huo umelenga kuhakikisha usalama wa Chakula hasa kwa mazao yanayovuka mipaka kwa kuhakikisha yanakuwa na ubora na kuhakikisha usalama wa chakula na FAO watatoa ushirikiano kuhakikisha mradi huo unatekelezeka na unaleta tija kwa kukuza sekta ya kilimo na mazao nchini na nje ya nchi.



Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI