BRELA: BIASHARA ILIYOSAJILIWA NI ULINZI WA MJASIRIAMALI


Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

WAJASIRIAMALI  wadogo na wa kati wameshauriwa  kuhakikisha wanasajili biashara zao kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kuwa huruna  kuwawezesha kupata fursa mbalimbali zikiwamo kupata mikopo kutoka za taasisi za kifedha pamoja na kulinda alama za biashara zao.

Hayo yalisemwa leo June18,2025   jijini hapa na Afisa Leseni Mwandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Koyan Abubakari, katika maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye Kaulimbiu isemayo"Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji"ambayo yanaendelea katika Viwanja vya Viwanja vya Chinangali Part.

Amesema kuwa katika maadhimisho hayo wakala huo upo kwa ajili ya kumsaidia mfanyabiashara kwa kutoa elimu ili aweze kuzihamu fursa zitokana na biashara zenye jina la biashara pamoja na Alama.

Afisa huyo ameeleza kuwa huo ni msingi bora wa biashara na silaha ya kwanza kwa maendeleo ya mjasiriamali yeyote hapa nchini huku akisema hiyo  ni hatua ya awali ya kujenga biashara imara na halali kisheria.

Ameongeza kuwa huduma zinazotolewa na BRELA katika maonesho hayo ni pamoja na usajili wa majina ya biashara kwa gharama ya shilingi 20,000, usajili wa viwanda vidogo, leseni za biashara na usajili wa alama za biashara.

Kwa upande wake mjasiriamali wa kushona nguo  aliyetembelea banda la BRELA Angelic Zavallah amesema kuwa awali alijua hatua za kusajili jina la biashara zinachukua muda mrefu.

"Huwezi amini nimekuja leo kusajili jina la biashara yangu haijachukua muda mrefu nimefanikiwa kwa sasa nimefurahi kwa kuwa ndio mwanzo wa hatua nyingine muhimu katika biashara," amesema.

Aidha amewashauri wajasiriamali kufika katika banda hilo kupata huduma ya usajili wa jina la biashara na kwamba  hakuna urasimu wowote.

Post a Comment

0 Comments

BRELA: BIASHARA ILIYOSAJILIWA NI ULINZI WA MJASIRIAMALI