SABAYA ASHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA MWENYEKITI WAZAZI WILAYA UBUNGO


 Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo Meshack Sabaya akizungumza mara baada kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo.

 Viongozi waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali ndani ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo.


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano  Mkuu Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo.

NA ASHA MWAKYONDE,DAR ES SALAAM

CHAMA cha Mapinduzi  (CCM),Wilaya ya Ubungo jana Septemba 25,2022 kimefanya uchaguzi wake wa  ndani ya Chama hicho wa Jumuiya ya Wazazi ambapo kura zimerudiwa kupigwa  mara tatu ili kumpata mshindi kwenye wa nafasi ya Uewenyekiti.

Akizungumza mara baada ya kutangaza  matokeo  Msamamizi Mkuu wa uchaguzi huo Edson Fungo amesema uchaguzi ulikuwa mgumu kutokana na wagomea  nafasi hiyo kura zao zikilingana idadi hivyo kushindwa kumpata mshindi.

Msimamuzi huyo amesema kuwa nafasi ya  mwenyekiti, mchuano wake ulikuwa mkubwa kwa kuwa wagomea wa nafasi hiyo Meshack Sabaya na mpinzani wake Justin Sanga ambaye alikuwa akitetea kiti chake  kura zao zilikuwa zinalingana idadi hali iliyosababisha uchaguzi huo kurudiwa mara tatu ili kumpata mshindi kwenye nafasi hiyo.

" Uchaguzi ulikuwa makini, mgumu kulikuwa na mpambano mkubwa sana katika nafasi ya uenyekiti, kupiga kura mara tatu sio jambo dogo kura zilikuwa zinagongana awamu ya tatu ndiyo tukampata mshindi, nawapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa Wilaya ya Ubungo wamefanya kazi iliyotukuka" amesema.

Msimamizi huyo  amesema nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na Sabaya ambaye amepata kura 159 kati ya kura  294 zilizopigwa , zikizoharibika ni tatu na kura halali ni 291  huku Sanga akapata kura 132.

Akizungumzia uchaguzi huo mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo  Sabaya ameeleza kuwa demokrasia katika Chama hicho imekuwa kubwa pamoja na uelewa wa wanachama kutokana na kurudia kupiga mara tatu katika uchaguzi huo.

Mwenyekiti huyo amesema wanachama hawakutaka kubahatisha ndiyo maana mchakato wa kupiga kura mara tatu umefanyika lengo lao ni kuhakikisha wanapata kiongozi ambaye wanajua atawatendea haki na kufanya kazi za Chama ipasavyo.

"Uchaguzi umeisha tuangalie jinsi ya kukijenga Chama kwa sababu tunajua kazi kubwa ilipo mbele yetu ifikapo 2025 si jambo dogo la kisiasa katika karne hizi, hivyo tuvunje makundi tufanye siasa zenye faida kwenye jumuiya hii. Nawashukuru sana imekuwa siku ndefu lakini wajumbe mmeweza kuvumilia," amesema.

Ameongeza kuwa viongozi waliochaguliwa watahakikisha wanafanya kazi kubwa ili hata waliowachagua wajue wanazitendea haki nafasi waliochaguliwa.

Kwa upande wake sanga aliyekuwa anakitetea kiti chake amewataka wafuasi wake wasiumie kwa kuwa ndio siasa huku akiwashukuru kwa kumstaafisha kwa heshima katika mpambano mkali wa kurudia kupiga kura mara tatu.

" Nawashukuru wapiga kura wote ambao wamenipigia na wasionipigia hii ndio demokrasia, kuwa na mawazo ya kusema we ndio kiongozi basi wewe sio mwanademokrasia ni lazima ukubali kushindwa na kushinda nashukuru mmenistaafisha kwa heshima katika mpambano uliokuwa mgumu,"amesema.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU