SEPESHA RUSHWA MARATHON KUFANYIKA DISEMBA 11 MWAKA HUU





Mwenyekiti wa mabalozi wa Taasisi ya Sauti ya Wapinga Rushwa (Anti-corruption Voices  Foundation - ACVF), Haruna Kitenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

NA ASHA MWAKYONDE,DODOMA

ZAIDI ya washiriki 2000  wa mbio za Sepesha Rushwa kutoka mikoa yote ya Tanzania wanatarajiwa kukimbia mbio za nusu marathon kilomita 21,10,5 na 3 lengo kuu likiwa ni kujenga uelewa wa kupinga rushwa  na kuhamasisha  sauti za jamii kuelimisha vijana dhidi ya rushwa hapa nchini.

Mbio hizo za marathon zimeandaliwa na Taasisi ya Sauti ya Wapinga Rushwa (Anti-corruption Voices  Foundation - ACVF), ikiwa na lengo la kutoa hamasa kwa vijana kama kundi maalumu  na Umma wa Watanzania kupinga vita vitendo vya rushwa  dhidi ya dhuluma na udanganyifu.

AVCF, inaomba udhamini na ushiriki wa serikali, Azaki, Taasisi za dini , sekta binafisi na wadau wapinga rushwa ili kufanikisha Sepesha Rushwa Marathon na kampeni yao ya "Badili Tabia" itakayoendelea kwa kipindi cha miaka mitatu kwa awamu ya kwanza.

Pia taasisi hiyo inaundwa na vijana wazalendo  wa kitanzania  waliomaliza  elimu zao katika ngazi mbalimbali kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu ambao wamelelewa kwenye vilabu vya wapinga rushwa wakiwa masomoni.

Akizungumza jijini hapa jana wakati wa kutoa ratiba ya mbio hizo Mwenyekiti wa mabalozi wa taasisi hiyo Haruna Kitenge amesema kuwa  malengo mahususi ni kukusanyasa na kuchangisha rasilimali fedha zitakazoisaidia taasisi hiyo kutekeleza kampeni ya "Sepesha Rushwa" katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Arusha kama mikoa ya majaribio kwa kipindi cha miaka mitatu ifikapo Disemba 31,2025.

Kitenge ameeleza kuwa lengo jingine ni kukuza sauti ya vijana kukomesha na kupiga vita rushwa nchini ifikapo Disemba 31,2025.

" Gharama za usajili  katika mbio hizo zimegawanyika katika makundi matatu kundi la  wanafunzi kuanzia 10, kila mmoja15,000 kila mmoja atatoa 10,000, watu wazima 25,000 nao kuanzia 10 kila mmoja 20,000  na VIP ni shilingi 80,000 nalo kuanzia watu 10 kila mmoja 70,000," amesema Kitenge.

Kwa upande wake Mlezi wa Mbio hizo za sepesha rushwa Hamad Ndee amesema kuwa Tangu enzi za Rais wa kwanza wa Tanzania Mwlmu Julius Nyerere alipinga vita rushwaa na kusema taasisi hiyo imeona kwa upana suala la rushwa kwa kuwa  limekuwa tatizo kwa nchi .

Aidha amewataka  watanzania kushiriki mbio hizo katika kutokomeza rushwa hapa Nchini.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU