IGP WAMBURA: TUMEUNDA OPERESHENI KABAMBE YA MSOKO WA PANYA ROAD

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)Camillius Wambura  amesema serikali imeunda operesheni kabambe ya msako ambayo itakayo kuchunguza na kuhakikisha nchi katika hali ya utulivu na amani.

Pia amewaonya  watu  wenye dhamira ya kujihusisha na matukio kiuhalifu yanayoweza kuvuruga amani ya nchi kuacha haraka kwa kuwa jeshi hilo limejipanga.

Hayo yamesemwa  Septemba  16, 2022 wakati akizungumza Wanahabari jijini Dodoma lengo likiwa kuelezea hatua za serikali katika hali ya ulinzi na usalama kufuatia matukio ya kihalifu hapa nchini amesema wanaoshirikiana na wahalifu hao hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

IGP Wambura amesema wao kama jeshi hawatakubali uhalifu ujirudie hivyo ni wakati mbaya kwa wahalifu hao huku akisema kuwa jeshi hilo halijawahi kushindwa. 

Ameongeza kuwa tayari iadi kubwa ya wahalifu wanaojiita Panya Road wameshawakamata  na kwamba bado wanaendelea na operesheni nyingine za ukamataji.

" Nawapa pole wale wananchi ambao wamepata majeraha ya kujeruhiwa na Panya Road pamoja na kuibiwa mali zao hivyo Kama hesho tunaendelea na msako wa wahalifu hawa," amesema IGP Wambura.

Awali  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amesema tayari wamekwisha weka mpango wa kupambana na wanaovuruga amani ya nchi Panya Road kwani uchunguzi umebaini wahusika wakuu ni wafungwa waliomaliza muda wao gerezani.

“ uchunguzi umebaini baadhi ya wafungwa waliomaliza muda wa kifungo chao ndio wanaoenda kuwashawishi vijana wengine mtaani niwaombe wananchi kutoa  ushirikiano katika ngazi zote hapa nchini kuanzia ngazi ya kata lengo letu ni  nchi ibaki salama," amesema Waziri huyo.

Ameongeza kuwa Suala la Ulinzi limeboreshwa kuanzia ngazi ya kata na kwamba jukumu la kulinda amani ya nchi ni kwa raia wote  huku akiitaka jamii  kuripoti vitendo vya kiuhalifu sehemu sahihi ambayo ni Jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI