WAZIRI AWESO: WIZARA HAITAMVUMILIA MTUMISHI ATAKAYEKWAMISHA UTEKELEZAJI

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema Wizara inafanya tathmini ya Wakurugenzi, Wahandisi na watumishi wa Wizara hiyo ambao hawatimizi wajibu wao na Wizara haitamvumilia mtumishi yoyote ambae atakwamisha utekelezaji wa miradi ya maji huku akiwataka kusimamia miradi ya maji kwakuhakikisha fedha za miradi zinaleta matokeo chanya.

Ameyasema hayo  leo jijini Dodoma  wakati akizindua programu ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya tatu amesema program ya kwanza haikufanya vizuri kutokana na baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu.

"Hatutaweza mvumilia mtu ambae hatasimamia  na atakwamisha miradi hii niseme ukweli  natoa rai  watumishi kufanya kazi kwa tija na kuhakikisha miradi inakua shirikishi"amesema Aweso

Awali wakizungumza kuhusu mchango wa sekta ya maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt James Mdoe amesema kupitia mradi huo watajenga vyoo bora na mabomba ya kunawia mikono katika shule za msingi 2800, sekondari 1400 na vyuo vikuu.

Kwaupande wake mwenyekiti wa kamati ya kilimo, mifugo na maji (Mbunge) Christina Ishengoma amesema licha yakuendelea kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa wananchi lakini jitihada zaidi zinahitajika sambamba nakuboresha utoaji bill za maji nakusikiliza malalamiko ya wananchi.

"Tunapoboresha na kusogeza huduma ya Maji kwa wananchi tujitahidi  kutatua na haya malalamiko ya  kuongezewa bill za maji hii imekuwa ni changamoto wananchi wanalalamika sana"amesema Ishengoma.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI