WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la sita la uwezeshaji Wananchi kiuchumi ambalo linatarajia kufanyika Septemba 19Mwaka huu Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo ambalo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
“Nitoe wito kwa wananchi wa Dodoma wajitokeze kuhudhuria katika kongamano hili ambalo litakuwa ni fursa kwao katika masuala ya uwekezaji na kama tunavyofahamu kwa sasa hapa makao makuu kwahiyo tujitokeze kwa wingi”amesema Senyamule.
Ameiongeza Dodoma ina miradi mingi ya uwezeshaji kiuchumi ikiwamo ya ile ya kilimo cha umwakigili ambacho vijana wengi wamejiingiza katika kilimo hicho huku akisema kuwa jijini hilo ni salama kwenye uwekezaji.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Beng’i Issa ameainisha lengo la Kongamano hilo kuwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi huku jopo la majadiliano la wakuu wa Mikoa litakuwepo pamoja na Wataalam.
Ameongeza kuwa kongamano hilo ni muhimu na pekee ambalo nchini inaenda kukaa kujitathimi katika sera yao uwezeshashaji wananchini kiuchumi hivyo kutakuwa na taarifa ya mwaka ya ambayo inaonesha wananchi walivyowezeshwa.
“Kutakuwa na tuzo ya mjasiriamali bora, taasisi bora za fedha, natoa fursa hii kuwakaribisha sana na tunaamini watu wengi watakuja Dodoma na kwa wale ambao hawatakuja kongamano hili
litaoneshwa mbashara,”amesema Katibu huyo mtendaji.
Kwa upanda wake Meneja wa Benki ya Stanbic Dodoma, Oppi Igolola amesema kuwa kongamano hilo ni fursa kwao Kama benki kushiriki katika mijadala ya ya kuchanganua ni namna gani wanaweza kuwawezesha wananchi ili waweze kushiriki katika fursa za biashara na uwekezaji.
0 Comments