Na Mwandishi Wetu, Dodoma
IKIWA leo ni siku ya mwisho ya kujadiliwa kwa bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wananchi mkoani Dodoma wamejitokeza kutoa maoni yao kuhusu bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 yenye kiasi cha shilingi bilioni 11.7.
Akizunguzmia bajaeti hiyo mkazi wa Dodoma Bi Maria Julias ambaye pia ni fundi cherehani amesema kuwa anatamani bajeti ya TAMISEMI ilenge zaidi kwenye TEHAMA ambapo itawarahisishia wafanyabiashara kwani dunia ipo kiganjani hivyo inawarahisishia wafanyabiashara kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii.
“Mfano mimi nikishona nguo zangu huwa naweka kwenye mitandao ya kijamii kwahiyo natumai tamisemi itatusaidia kwa upande huo”amesema Maria.
Kwa upande wake Emmanuel Mabalwe amesema kuwa amefuatilia Bunge na kuona bajeti ya Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyowasilishwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe Mohammed Mchengerwa.
0 Comments