WAKAZI 350 WA TANGA KUPATIWA HUDUMA YA UPASUAJI WA MABUSHA

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WiZARA ya Afya imesema kuwa imeanza mkakati wa kukabiliana na magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele ili kuweza kuyatokomeza  ifikapo Mwaka 2030 ambapo inatarajia kutoa huduma ya upasuaji wa mabusha (Operation) kwa wakazi 350 Katika Mkoa wa Tanga na watafika mpaka Mkoa wa Mtwara ili kuendelea kutoa huduma hiyo.

Hayo yameelezwa leo Janauari 27,2023 Jijini Dodoma na Meneja Programu wa Mpango wa Taifa wakutokomeza magonjwa yasiyo pewa kipaumbele, Dk.George Kabona Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambayo yanatarajiwa kuadhimishwa Januari 30 Mwaka huu Mkoani Tanga

Ameelezakuwa   katika tafiti iliyofanyika awali, Ugonjwa huo ulikuwa katika Halmashauri 119 hapa nchini na kwamba  walifanikiwa kugawa dawa katika Halmashauri zote.

Dk. Kabona amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata matibabu ya magonjwa hayo kwenye kambi za matibabu pamoja na umezaji wa dawa.

Naye Afisa Programu mabusha na Matende Oscar Kaitaba ametoa rai kwa  wananchi kuweka mazingira katika hali ya usafi,kuua mazalia ya mbu na kulala kwenye chandarua .

Kwa upande wa Programu Ofisa wa Magonjwa ya Kichocho na Minyoo ya tumbo toka Mpango wa Taifa wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele,Mohamed Nyati 
amesema kwa Tanzania Mwaka 2004 ilionekana Halmashauri zote184 na Mikoa yote iliathirika na kichocho na kusababisha utapiamlo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI