WAZIRI NAPE AUNDA KAMATI YA KUTATHIMINI HALI YA UCHUMI KWA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

WIZARA ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeunda kamati ya Watu 9 ambayo inaongonzwa na Mwenyekiti wake Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group Tido Mhando
yenye lengo la kutathimini hali ya uchumi  na utendaji katika vyombo vya habari.

Akizungumza na waandishiwa habari jijini hapa leo,Januari 24,2023,Waziri wa Wizara hiyo Nape Nnauye amesema wakati Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha alimwagiza kuangalia hali za uchumi na utendaji  wa vyombo vya habari  na hali ya  kiuchumi .

Waziri Nape amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo  Rais Dk.Samia haridhishwi na uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari na kumuagiza namna ya kushughulikia tatizo hilo 

Nape Katibu wa kamati  hiyo  ni Msemaji  Mkuu wa serikali Gregson Msigwa  na wajumbe ni Mkurugenzi Mkuu wa TAMWA, Dk.Rosse Rubeni,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One,Joyce Mhavile, Mjumbe,Sebastian Maganga, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL,Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Sembeya, Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice,Jackiline Owiso huku akimuongeza  mjumbe mwingine ambaye ni mwandishi wa habari ,Richard Mwaikenda.

"Kamati hii  inatakiwa kuwa imekamilisha kazi ndani ya miezi mitatu sawa na siku tisini na  kazi kubwa ya kamati  kufanya tathimini ya hali ya uchumi kwa vyombo vya habari kielimu na kiutendaji ,hali ya waandishi wa habari na vyombo vya habari ikiwa pamoja ajira,vipato,mikataba na wawakilishi waliopo mikoani," amesema Waziri Nape.


Ameongeza kuwa kamati hiyo itatakiwa kutoa taarifa kwa jinsi utekelezaji wa mikataba na ajira vinavyo heshimi na  kutafuta changamoto inayosababisha changamoto ya kiuchumi na changamoto ya kutekeleza kupitia vyombo vya habari serikali na wadau.

Waziri huyo ameeleza kuwa kazi ya kutafuta maoni ni ya watu wote hivyo watanzania pamoja na wanahabari wanatakiwa kutoa ushirikiano wa kutoa maoni kwa njia ya Mtandao na kwamba mchakato wa mabadiliko ya sheria ya huduma ya vyombo vya habari umefikia pazuri tayari umeshapelekwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Akizungumzia  kuwepo kwa matapeli amesema zaidi ya milioni 2, hazijahakikiwa hivyo kutokana hali hiyo zitafungiwa kwa kuwa zinatumika vibaya kutapeli wananchi.

Waziri Nape amesema ambao wanatumia laini za simu vibaya ifikapo mwenzi ifikapo Februari 13 mwaka huu saa kumi jioni laini zote ambazo hazijahakikiwa zitazimwa na kwamba zaidi ya laini za simu milioni 60 zimesajiliwa na zaidi ya milioni 58 zimehakikiwa.

Hata hivyo ametoa wito  kwa watanzania kuhakikisha kila mwenye laini ya simu na hata kama kuna mtu ambaye alisajiliwa laini yake na ndugu yake kwa kutokana na changamoto ya Mamlaka ya Vitabulisho vya Taifa (NIDA) ni wakati mzuri  wa kufanya uhakiki na  zikifungiwa hazitafunguliwa.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI