BMH NA KUWAIT YASAINI MAKUBALIANO YA HUDUMA YA UPASUAJI WA MAGONJWA YA MOYO KWA WATOTO


 Na  Asha Mwakyonde,Dodoma

JOPO la Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, wauguzi na wataalam wa huduma za matibabu ya Moyo kutoka  nchini Kuwait wamewasili katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), kwa lengo la kutoa huduma ya Uchunguzi  wa magonjwa hayo na tayari watoto wawili wameshafanyiwa upasuaji na jopo hilo baada ya kugundilika kuwa na tatizo la Moyo.

Pia Hospitali hiyo imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za Upasuaji wa Moyo kwa watoto na Shirika lisilo la kiserikali la Children Heart Charity Association la nchini Kuwait

Akizungumza jijini Dodoma katika hospitali hiyo leo Februari 6,2023 mara baada ya kusaini makubaliano hayo makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Alphonce Chandika ameeleza kuwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo umeanza tangu Februari 3 na unatarijiwa kumalizika Februari 9 mwaka huu.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa wanatarajia kuwafanyia uchunguzi watoto 100  pamoja na kuwapatia matibabu kwa watakaogundulika kuwa na tatizo la moyo huku akishukuri nchi 
Kuwait kwa ushirikano wao wa kutibu magonjwa ya moyo kwa watoto.

Amefafanua Hospitali hiyo awali ilikuwa inatibu watoto 400 kwa mwezi  na kwamba kwa sasa watakuwa na uwezo wa kutibu watoto 3400.


Dk. Chandika, Akizungumzia maeneo waliyokubaliana  na nchi hiyo amesema yapi matatu ambayo ni kugharamia watoto wenye matatizo yanayohitaji Upasuaji wa moyo,kuwezesha vifaa tiba vinavyohitajika kwenye matibabu ya moyo pamoja na kuwajengea uwezo madaktari,wauguzi na wataalam wa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa  hayo katika hospitali hiyo.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Said Musa amesema ujio wa madaktari hao bingwa hapa nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za moyo kwa watoto ikiwemo Upasuaji.

Amesema anaishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kutokana na ushirikiano waliotoa kwa madaktari hao na kuwataka waendelee kuwa na Moyo wa utoaji matibabu ya Moyo.

Kwa upande wake Dr Faisal Al-Saied amesema wanaimani malengo wanayotarajia kuyafikia yatafanikiwa kwa sababu wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa Hospitali hiyo.

"Jamii inapaswa ijitokeze kwa  wingi Ili kupata huduma ya uchunguzi pamoja  na kupata matibabu ya Moyo kwa watoto wadogo hususani wale wanaohitaji Upasuaji," amesema.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU