JKT: YAKANUSHA PICHA ILIYOTUMIKA KATIKA TAARIFA YA VIJANA 147 WENYE MAAMBUKIZI YA VVU


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

JESHI la kujenga Taifa (JKT),limesema  kuwa picha iliyotumika katika  taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari ikionesha vijana wa Jeshi hilo 147 wanamaambukizi ya VVU ni ya vijana wanaoendelea na mafunzo yao na kwamba taarifa iliyoelezwa haina mahusiano yoyote na picha hiyo.

Pia Jeshi hilo linavitaka vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii vilivyoripoti habari hiyo kwa kuweka picha za vijana wa JKT ambao si wahusika kuomba radhi na kuondoa picha hiyo mara moja.

Akizungumza jijini Dodoma leo Februari 6,2023 wakati akikanusha na kufafanua kuhusu picha hiyo, Mkuu wa Tawi la utawala  wa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema  Kamati ya Bunge ambayo inahusiana na masuala ya ukimwi  ilitoa taarifa yake Februari 3,2023  bungeni ikielezea jinsi maambukizi yalivyo  na hali ilivyo  katika kutoa takwimu mbalimbali.

Brigedia Jenerali Mabena amesema Kamati hiyo iligusia wale vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha sita na kwenda kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo kuwa wanapimwa.

Amefafanua kuwa katika kipindi  Cha mwaka wa fedha 2018 hadi 2021 walibainika vijana 147 kuwa na maambukizi ya ukimwi  kwa baadhi 
yao waliomaliza kidato cha sita kutoka shule mbalimbali wanaoenda kufanya mafunzo ya lazima na kwamba wakifika katika kambi za Jeshi hilo wanapimwa afya zao.

"Katika kupimwa afya zao ndiyo ile idadi taarifa yake imetolewa bungeni ndiyo waliobainika kuwa vijana hawa 147 wameambukizwa ni ya kipindi cha miaka mitatu," amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Ameongeza kuwa mafunzo ya vijana wa kundi la lazima (wahitimu wa kidato cha sita), huendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu na kabla ya kuanza mafunzo hayo hufanyiwa usahili wa nyaraka zao pamoja na vipimo vya afya  ili kufahamu utimamu wa mwili ( physical Fitness).

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI