WATOTO WACHANGA WANAOPEWA MAZIWA YA NG'OMBE WAPO HATARINI KUPATA KISUKARI


 Na Asha Mwakyonde

DAKTARI Mkaazi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kitivo cha Afya, Maseto Galikunga amesema kuwa moja ya sababu zinazotajwa kwa watoto kupata hatari ya tatizo la ugonjwa wa kisukari ni kupewa maziwa ya ng'ombe wakiwa wachanga bila kuchanganywa na maji.

Akizungumza Jijini Dodoma  Dk.Galikunga kwenye mahojiano maalumu katika  Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma, amesema tabia hatarishi zinazoweza kusababisha kundi la watoto kupata ugonjwa wa kisukari ni akina mama huona maziwa ya ng'ombe  ni rahisi kuyapata kuliko maziwa ya kisasa ya kopo.

Daktari huyo amefafanua kuwa maziwa ya ng'ombe ni mazito na kusababisha kongosho lifanye kazi kuliko kawaida kutoa kichochoe cha Insulini ili yaweze kumengenywa.

"Baadae seli za kongosho zinaharibika kidogo kidogo  kufa na kusababisha mtoto huyu baadae aweze kupata tatizo la ugonjwa wa kisukari," amesema Dk. Galikunga 

Daktari huyo amesema kuwa kuwapa watoto vyakula vingi kupita kiasi, vyenye sukari nyingi vinaweza kuwasababishia unene kupita kiasi na wenye uzito wa kupitiliza ni kuwaweka watoto hao kwenye hatari ya kupata tatizo la sukari.

Aidha Dk.Galikunga ametoa wito kwa wazazi wasipende kuwapa watoto chakula kingi kupitiliza, vyenye sukari nyingi na kwamba wanapowaandalia watoto hao chakula wahakikishe  wanawapatia makundi yote muhimu ya cha chakula.

Dk. Galikunga meyataja makundi hayo ya vyakula kuwa  ni kundi la Wanga,prorini , vitamini, madini na vile vyenye mafuta .

Ameseisiza kuwa kila kundi lina umuhimu wake katika kujenga mwili, kuukinga na kusaidia kuepusha magonjwa pamoja na kusaidia seli za mwili ziweze kurudi katika ubora wake.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya  
asilimia 97 ya watoto wanaozaliwa hunyonyeshwa maziwa ya mama, ikiwa asilimia 92 ya watoto hunyonyeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuendelea.

Na kwamba asilimia 43 tu ya watoto ndio hunyonyeshwa hadi kipindi cha miaka miwili na kuendelea huku takwimu zikionesha asilimia 57 ya watoto ndiyo hunyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kuchanganya na chakula kingine wala maji ndani ya kipindi cha miezi 6.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI