MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Juni 5, mwaka huu saa 6:01 usiku.
Pia wafanyabiashara wametakiwa kuuza bidhaa za mafuta kama kwa bei husika zilizotololewa na mamlaka hiyo na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka agizo hilo.
Katika taarifa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURADk.James Mwainyekule ilisema kuwa kwa mwezi Juni 2024, bei za rejareja na za jumla katika mikoa ya Dar es Salaam,Tanga na Mtwara ambapo bei kikomo za rejareja kwa lita.
Amefafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam petroli ni shilingi Dar es Salaam 3261, dizeli 3,112, mafuta ya taa 3,261 Tanga petroli 3,263, dizeli 3,221, mafuta ya taa 3,307 na katika Mkoa wa Mtwara petroli 3,267, dizeli 3,222 na mafuta ya taa3,333.
Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa bei kikomo za jumla katika bandari za Dar es Salaam petroli ni 3,128.72, dizeli 2,979.99, mafuta ya taa 3,128.69, Tanga Petroli 3,131.14, dizeli 2,988.78 na Mtwara petroli ni 3,134.43, dizeli 2,989.84.
Kwa mujibu mkurugenzi huyo mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Juni 2024 yamechangiwa na kupungua kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 11.82 kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.77 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 7.94 kwa mafuta ya taa.
"kuongezeka kwa wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) kwa asilimia 1.4 kupungua kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums), amesema na kuongeza.
Kwa kusema wastani wa asilimia 2.06 kwa petroli na asilimia 8.51 kwa dizeli katika Bandari ya Dar es Salaam; kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 7.07 kwa petroli na asilimia 25.24 kwa dizeli katika Bandari ya Tanga," ameeleza Dk. Mwainyekule.
Amesema zimepungua kwa wastani wa asilimia 12.64 kwa mafuta ya petroli na 12.61 kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara ambapo Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zilizoorodheshwa na mamlaka hiyo.
Dk.Mwainyekule ameeleza kuwa wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei kwa mujibu wa bei zilizopangwa.
Amesema EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii ambapo bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.
"Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini na kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko," alisema.
Ameongeza kuwa EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap),au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa
Kanuni za EWURA za kupanga bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Namba. 57 na marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Namba 761A la Oktoba 30, 2023 na Mabadiliko ya kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za mwaka 2024.
Amesema vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.
"Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani .Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja," amesema.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika na kwamba Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.
Amefafanua kuwa Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa.
Mkurugenzi huyo ameeleza Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.
0 Comments