KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAPITISHA BAJETI YA TACAIDS

Na Mwandishi wetu- DODOMA

KAIMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Dkt Christina Mnzava ameipongeza Serikali kwa kuongeza bajeti katika Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) ili kuendelea kusimamia Afua kwa kutumia fedha za ndani.

Dkt. Mnzava ametoka pongezi hizo leo tarehe 24 Machi, 2025 Jijini Dodoma wakati wa kupitishwa taarifa ya utekelezaji wa mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024-2025 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025-2026 kwa fungu 92 Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inayofanya majukumu yake chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu

“Nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuongeza fedha katika mfuko wetu ni hatua nzuri sana, niwasihi watendaji wa Serikali kuendelea kufuatilia fedha hizi ili mipango tuliojiwekea iweze kutekelezwa kwa usahihi,” alisema Dkt. Mnzava.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Willliam Lukuvi alibainisha kwamba kulingana na hali ya sasa ya usitishwaji wa misaada kutoka fedha za nje, serikali imejipanga kuendelea kutekeleza AFUA muhimu zenye tija na kuleta matokeo makubwa ifikapo mwaka 2030.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania Dkt. Catherine Joachim amesema tume iliidhinishiwa muundo mpya ambao ulifanya Tume ya Kudhibiti Ukimwi kuwa na  vitengo saba na ofisi za kanda saba .

Aidha alieleza kwamba ili kuimarisha uratibu Mameneja wa Kanda ambao wako chini ya Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa watajengewa uwezo ili waweze kutembelea mikoa ambayo wanairatibu.





Post a Comment

0 Comments

WAUGUZI, WAKUNGA ENDELENI KUBEBA DHAMANA KAMA SERIKALI ILIVYOWEKEZA