KIKAO CHA KAMISHENI MPYA YA TUME YA MADINI CHAFANYIKA

📍Mikakati kabambe yawekwa katika kuinua Sekta ya Madini

Dodoma 

KIKAO cha Kamisheni ya Tume ya Madini leo Disemba 05, 2024 kimefanyika kikao cha kwanza  

tangu kuteuliwa kwa Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo, Janet Lekashingo ambacho kimeshirikisha Makamishna wa Tume na Menejimenti.

Lengo la kikao hicho ni kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo mwaka.  

Akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao hicho Mwenyekiti huyo Lekashingo amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Madini hasa kwenye eneo la ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa nchini, kuimarika kwa usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na mchango wa kampuni za madini kwa Jamii.

Kupitia kikao hicho mikakati mbalimbali imewekwa kupitia Kamati za Ufundi, Rasilimaliwatu, Fedha na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini.







Post a Comment

0 Comments

KAMATI MAALUM HUDUMA YA AFYA YAUNDWA MAANDALIZI YA AFCON