📍Watanzania watakiwa kujitokeza kwenda Mombasa, Kenya kuishangilia.
Na Asha Mwakyonde DODOMA
MWENYEKITI wa Bunge Sports Clab Tarimba Abbas ameeleza kuwa timu ya Bunge la Tanzania inatarajia kushiriki mashindano ya mchezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Disemba 7, mwaka huu Mombasa nchini Kenya.
Hayo ameyasema leo Disemba 4, 2024 jijini Dodoma bungeni wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mashindano hayo yanatarijiwa kuanza Disemba 7, mwaka huu.
Amesema kuwa mashindano hayo yatamalizika Disemba 17, na kwamba timu ya Bunge Sports Club imejiandaa vema ambapo ilikuwa kabimbini kwa muda wa wiki mbili.
"Timu inatarajia kuondoka nchini Disemba 6 na itakuwa na watu 20 ambao watashiriki michezo mbalimbali," ameeleza Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo ameitaja baadhi ya michezo kuwa ni mpira wa kikapu, wavu , kuvuta kwamba pamoja na mchezo wa vishale (Darts), maalum kwa wabunge wenye ulemavu na mchezo wa Golf kwa wanawake na wanaume huku akisema mashindano hayo ni ya 14 tangu kuanzishwa.
Aidha amezitaja nchi ambazo zitashiriki mashindano hayo kuwa Tanzania, Kenya ambao ni wenyeji, Rwanda, Burundi Uganda, Sudani Kusaini, Somalia na DRC Kongo.
Amefafanua kuwa lengo la mashindano hayo ni kuimarisha mahusiano katika nyanja mbalimbali na kwamba timu hiyo inatarajia kurejea nchini Desemba 18, mwaka huu.
"Tanzania hatuaendi kama washiriki tu bali tunaenda kwa ajili ya kushinda,tumekuwa tukifanya vizuri katika mashindano haya," ameeleza Tarimba.
Naye Meneja wa Bunge Sports Club ambaye ni mbunge wa Jimbo La Manonga, Tabora Seif Gulamali amewataka watanzania wanaoishi Mombasa, Kenya na maeneo ya karibu kujitokeza kwa wingi kwenda kuishangilia timu hiyo.
Ameongeza kuwa timu hiyo imekuwa ni hatari katika mashindano hayo na kwamba wanaamini watarejea nchini wakiwa na makombe ya ushindi.
0 Comments