SHULE YA UONGOZI KIBAHA YAWAPANGA KWA UPYA VIJANA VIONGOZI KWA USHINDI WA CHAGUZI ZIJAZO


Kibaha, Pwani 

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara John Mongella amesema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita hivi karibuni ni kwa sababu chama hicho kilitumia vijana kwenda kuambia vijana wenzao namna ambavyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilichofanya kwenye jamii nchini.

Amesema hayo mjini Kibaha mkoani Pwani wakati akifungua mafunzo ya 13 ya uongozi ya mapitio ya juhudi za kuleta mabadiliko ya kisasa katika nyanja za maendeleo yaliyohusisha vijana viongozi kutoka nchi 6 za kusini mwa Afrika katika harakati za maendeleo yaliyofadhiriwa na chama cha kikomunisti cha nchini China CPC.

Amesema vijana ni kundi lenye nguvu katika jamii na CCM ilipobaini hilo iliwapa jukumu hilo la kwenda kusema yaliyofanywa na serikali yao katika jamii.

"Ndio sababu CCM tuliamua vijana wafanye kazi ya kuelimisha jamii yaani serikali ya CCM imefanya nini, sisi tumeamua, sekretalieti ya CCM iliamua na Chama chetu sasa kimeamua ndio kinashikiliwa na vijana" alisema 

"Lakini naamini Kazi kubwa sasa ni kuunganisha vijana wote kwani wanaweza kusaidia chama kwenye jamii hivyo inahitajika nguvu kubwa ya kuunganisha vijana wengi zaidi na wazee wengi zaidi wenye kusaidia chama na kusaidia jamii yaani changamoto kubwa Afrika na dunia nzima ni kuwaunganisha vijana wote na hiyo ndio changamoto ya vyama vyote sita vya ukombozi, Afrika nzima kwani bara Afrika inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vijana" alisema. 

Awali Mongella alianza kwa kupongeza nchi ambazo zimeshakamilisha hatua za michakato ya uchaguzi na kupata ushindi wa kupata tena nafasi za kuongoza nchi zao.

"Niwapongeze sana wenzetu ambao tayari wamepita katika chaguzi ANC cha Afrika kusini, FRELIMO cha nchini Msumbiji, wenzetu wa SWAPO huko nchini Namibia kwasababu pamoja na changamoto zilizopo lakini chaguzi zimekamilika na sisi Taanzania juzi tarehe 27 tumekamilisha uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo CCM ilishinda kwa takribani zaidi ya asilimia 98" alisema Mongella.

Alisema Vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa baada ya uchaguzi vinatakiwa kurudi kwa Wananchi hususani kwa kwenda kwa vijana kwa lengo la kuendelea kuwajenga vijana kwani ni lazima kuwa na vijana ambao ni mfano kwenye jamii.

"Vyama vyetu vinatakiwa kurudi kwa wananchi kwani tunatakiwa kuwa na vijana ambao watakuwa na mvuto kwa wananchi ambao hasa kwakuwa vijana ndio kundi lenye idadi kubwa katika nchi zetu" alisema Mongella.

"Kama mnavyojua vyama vyetu sita vya ukombozi vilitaka tuwe na shule ya akujenga viongozi wenye mwelekeo wa aina moja katika nchi zote sita baada ya kufanya ukombozi uliofanywa na nchi zetu ilikujikomboa kiuchumi badala ya ukombozi uliofanywa na Wazee wetu wakutupatia uhuru nchi zetu" alisema Mongella.

"Ndugu zetu wa China tulikuwa nao tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru tupo nao mpaka hivi leo kwani Wazee wetu walikwishatimiza wajibu wao sasa zamu yetu kuzikomboa nchi zetu kiuchumi jambo ambalo ni kazi kubwa sio ndogo" alisema Mongella.

"Tumeona chaguzi kwenye nchi zetu zilivyokwenda ujumbe mkubwa ni kwamba vyama vyetu vinatakiwa kurudi kwa wananchi, vyama vyetu vinatakiwa kuwa na mvuto kwa vijana ambao ndio kundi lenye idadi kubwa katika nchi zetu ndio maana hata katika mafunzo haya vyama vimeleta vijana tu kwasababu vinajua vijana ndio mnaweza kuzungumza vijana wengine hivyo tunawategemea" alifafanua Mongella.

"Vyama vyetu lazima tuwe na vijana wenye mvuto na wenye sifa katika jamii hivyo niwaaombe vijana mjifunze sana na katika uzoefu mtakao upata hapa kwa Wazee na watoa mada watakao wafundisha; tuchukue nafasi ya kujifunza ili tuwezekushinda hii harakati zetu za kufanikisha nchi zetu kupiga hatua za maendeleo na kushinda katika chaguzi zilizo mbele yetu"

"Tujenge umoja utakao dumu kwa kujenga ushirikiano wa maendeleo hapo baadae"

Mkuu wa Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere Profesa Marcelina Chijoriga amesema mafunzo hayo ni mafunzo ya 13 kwa viongozi vijana kutoka nchi hizo sita zilizoshiriki harakati za ukombozi na kufadhiriwa na chama cha Kikomunisti cha nchini China CPC tangu kuanza kwa kutolewa mafunzo katika shule hiyo.

Profesa Chijoriga alisema walengwa wa kubwa wa mafunzo hayo ni vijana ambapo kila chama kimeleta washiriki 20 na kufanya jumla ya washiriki zaidi ya 100.

Alisema shule hiyo imeshatoa jumla ya mafunzo 62 kwani mafunzo mengine kwa watumishi wa taasisi za umma yametolewa shuleni hapo kuwa ni zaidi ya 49  tangu shule ilipooanza.

Naye Mwakirishi wa CPC ambaye ni Mkurugenzi wa Masuala ya bara la Afrika Liong Anping amepongeza ushirikiano uliopo katika nchi hizo sita zilizoshiriki katika harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa nchi hizo.

Post a Comment

0 Comments

MABADILIKO YALETA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA TANZANIA