MPANGO WA MACHO IMARA WAZINDULIWA DODOMA

📍Watoto nane kati kati ya 10,000 wana ulemavu wa kutokuona

Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

INAKADIRIWA kuwa wastani wa watoto nane kati ya 10,000 wenye umri wa miaka 0 hadi15, wana ulemavu wa kutokuona na idadi kubwa zaidi wana upungufu wa kuona.

Hayo amesemwa leo Februari 20,2025 jijini Dodoma Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Nchini ,Ziada Sellah ,wakati wa Uzinduzi wa mpango wa Macho Imara na wenye kaulimbiu isemayo "Uoni Bora,maisha bora"amesema Tanzania magonjwa ya macho bado ni changamoto kwa rika zote.

Amesema magonjwa hayo duniani yanaongezeka ambapo Shirika la Afya Duniani (WHO), linakadiria hadi sasa takribani watoto milioni 1.4 wanaulemavu wa kutokuona na kiasi cha asilimia 50 kati yao wanaoishi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mradi huo unatekeleza katika mikoa minne ya Tabora, Arusha, Singida na Manyara ambao utasaidia kuongeza wigo kwa ujumuishwaji wa huduma za afya ya macho kwa watoto.

Awali Mtafiti wa Mradi huo Profesa Milka Mafwiri amesema kuwa watoto milioni 1.4 duniani kote wanatatizo la macho na kwamba nusu ya watoto hao wanaoishi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Ameongeza kuwa tatizo hilo linasababisha zaidi na ukosefu, upungufu afua za utambuzi wa mapema kwenye huduma za mama na mtoto katika afya ya msingi.

Mtafiti huyo ameeleza kuwa watoto wanaofika katika matibu afya ya msingi hawapati vifaa na tiba stahiki kwa wakati.

"Sisi kama watafiti kuna kazi za awali ambazo tumezifanya kabla ya (leo), jana tulizianza tangu mwaka 2010 ambapo kulikuwa na hospitali mbili zilizokuwa zikiendesha huduma za macho kwa watoto za Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na Hospitali ya CCBRT," ameeleza.

Ameeleza kuwa changamoto wanayokutana nayo ni watoto kucheleweshwa kufikishwa katika vituo vya kutolea huduma ambapo wanafiki wakiwa na umri wa miaka tisa hadi 15 ambapo wakifanyiawa upasuaji tatizo lake anaendelea kuwa mlemavu.

Naye Afisa afya ya mama na mtoto ambaye ni mwakilishi wa WHO, Edwin Swai amesema kuwa wataendelea kushirikiana katika mradi huo ili kuhakikisha unatekelezwa kama ilivyopangwa.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: TANZANIA SIO SOKO LA DAWA ZA KULEVYA