Na Asha Mwakyonde,DODOMA
MBUNGE wa Kibiti Twaha Mpembenwe leo bungeni amuliza swali la nyongeza ambapo ametaka kujua lini barabara ya Bungu -Nyamisati itajengwa.
Amesema "wapiga kura wa Bungu na Nyamisati wanataka kujua lini barabara ya Bungu- Nyamisati itajengwa ikizingatiwa kwamba upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umeshafanyika.?"amehoji Mpembenwe.
Akijibu swali hilo jijini Dodoma leo Februari 7,2025 Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameeleza kuwa tayari serikali imeshafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Bungu-Nyamisati katika Jimbo la Kibiti mkoani Pwani.
Mhandisi Kasekenya amesema tayari walishaanza hatua ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.
"Nimwombe Mbunge tuonane kwa sababu kipindi hiki ndio tunaandaa mipango kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti inayokuja Ili tuweze kuingiza kwenye mipango ya bajeti ya 2025/26," ameeleza.
0 Comments