Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MAMALAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), imewahimiza Watanzania Kujisajili kwenye Mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma yaani National - e - Procurement System, (NeST), kwa lengo la Kushiriki Zabuni zinazotolewa na Serikali.
Hayo yameyasemwa leo Julai 5, 2025, na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Denis Simba, aalipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba' amesema watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa za kupata zabuni za serikali kwa kujisajili kwenye mfumo huo.
Amesema mfumo huo wa NeST upo unalenga kupata zabuni za serikali kwa uwazi ushindani ulio sawa.
Mkurugenzi Mkuu huyo ameeleza kuwa ili wafanyabisahara , watanzania waweze kunufaika na fursa mbalimbali za zabuni zinazotolewa na Serikali, hususan zabuni za asilimia 30 zinazolengwa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.l ni vema wakajisaji kwenye mfumo wa NeST ambao inaonesha uwazi katika upatikanaji wa zabuni serikalini.
"Mfumo wa NeST hauchagui uwezo wa mtu bali unaangalia vigezo vya muombaji hivyo Mtanzania yeyote mwenye sifa anaweza kuomba zabuni ya ununuzi serikalini,"amesema.
Simba amewataka watanzania kufika katika banda hilo kwa ajili ya kupata elimu ya namna ya kujisajili na kuomba zabuni za serikali kupitia mfumo huo.
0 Comments